Halmashauri ya Wilaya ya Songea inatekeleza Mpango huu wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu kipindi cha pili na ulianza kutekelezwa rasmi mnamo February 2020.
Lengo la mpango huu wa kunusuru kaya maskini ni kuwezesha kaya maskini kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharimia mahitaji muhimu kwa kupitia vikundi vya kuweka na kuwekeza vya walengwa, kusaidia kaya maskini za wazee, watoto waliojiandikisha shule na wale walio chini ya miaka mitano na kaya za watu wenye ulemavu.
2.0.1. UTOAJI WA RUZUKU KWA WALENGWA.
Halmashauri ya Wilaya ya songea imeanza utekelezaji wa mpango huu kunusuru kaya maskini mnamo mwaka 2015 kwa kutoa ruzuku ya TASAF kwa walengwa waapatao 5,257 kutoka katika vijiji 56.
2.0.2 MIRADI YA KUTOA AJIRA YA MUDA KWA WALENGWA
Halmashauri ya wilaya ya songea inatekeleza miradi ya kutoa ajira ya muda kwa walengwa, mirdi hii huibuliwa na wananchi kupitia mikutano maalum ya vijiji ya wananchi wote na hutekelezwa na walengwa wa mpango kwa lengo la kuongeza kipato kwa kaya.
Miradi hii hutekelezwa Zaidi kipindi cha ARI, ni kipindi ambacho kinakuwa kigumu kwa walengwa kupata mahitaji yao inavyotakiwa. Kwa halmashauri ya wilaya ya songea hutekeleza miradi hiyo kuanzia mwezi Sept kila mwaka na hukamilika mwezi februari kila mwaka.
Mpango huu wa utekelezaji wa miradi ya kutoa ajira ya muda kwa walengwa ni wa kipindi cha miezi sita (6) na kila mwezi walengwa hufanya kazi siku kumi, kwa masaa manne tu kila siku, na hulipwa shilingi 3,000 kila siku ambayo mlengwa atafanya kazi.
Miradi hii hutekelezwa kila kijiji na aina miradi inayotekelezwa ni ujenzi wa vivuko vya watembea kwa miguu, uboreshaji wa visima vya asili, uboreshaji wa barabara za mashambani, uanzishwaji wa mashamba ya korosho, uanzishwaji wa mashamba ya parachichi na utengenezaji wa pavement block ambazo zimewekwa kwenye sekondari na zahanati.
2.0.3. MIRADI YA UJENZI WA MIUNDO MBINU MBALIMBALI
Halmashauri ya wilaya ya songea imetekkeleza na inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali nayo ni kama ifuatavyo;
2.0.4 MPANGO WA UWEZESHWAJI KIUCHUMI WALENGWA (PRODUCTIVE GRANT)
Halmashauri ya wilaya ya songea inatekeleza mpango katika vijiji 36 kati ya vijiji 56. Mpango huu TASAF inawapa walengwa wenye uwezo wa kufanya kazi ruzuku ya uwezeshwaji kiuchumi kiasi cha 350,000 kila mlengwa kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali. Katika halmashauri ya wilaya ya songea jumla ya walengwa 1,676 wamepewa ruzuku hii na wameanzisha shughuli za uzalishaji za ufugaji wa kuku, mbuzi, nguruwe, mama lishe na kilimo cha mbogamboga.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa