DIVISHENI YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
Lengo kuu la divisheni
Kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa maendeleo ya viwanda, biashara, masoko na uwekezaji
Divisheni ya viwanda biashara na uwekezaji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea inaongozwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea chini ya mkuu ya Mkuu wa divisheni na wasaidizi wake.
Divisheni imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni
Divisheni ya Viwanda, Biashara, na Uwekezaji katika shughuli zake inatekeleza majukumu yafuatayo;
Sehemi hii katika utekelezaji wa majukumu na shughuli zake itaongozwa na Afisa mfawidhi wa maendeleo ya Viwanda na Uwekezaji, pia inatekeleza shughuli zifuatazo ndani ya divisheni ya Viwanda, Biashara, na Uwekezaji;
Kuratibu utekelezaji wa sera, sheria, kanuni na taratibu za sekta ya viwanda na uwekezaji;
Kukuza na kuratibu utekelezaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi;
Kutenga, kuendeleza na kufuatilia maeneo ya viwanda na hifadhi;
Kutoa ushauri kuhusu uboreshaji wa sera za Viwanda na kuratibu mikutano ya kisekta;
Kukuza uzalishaji wa malighafi mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya viwandani;
Kutayarisha na kutunza rejista za viwanda na vitega uchumi;
Kupanga na kukadiria ushuru kwa viwanda vidogo;
Kuendeleza na kupitia upya wasifu wa uwekezaji;
Kukuza uwekezaji wa sekta binafsi;
Kuratibu na kutoa ushauri kwa wawekezaji; na
Kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Sehemu hii katika utekelezaji wa majukumu na shughuli zake itaongozwa na Afisa mfawidhi wa Biashara na Masoko, pia inatekeleza shughuli zifuatazo ndani ya divisheni ya Viwanda, Biashara, na Uwekezaji;
Kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, kanuni na taratibu za biashara na masoko;
Kutoa ujuzi wa ujasiriamali kwa jumuiya ya wafanyabiashara;
Kuratibu na kutoa ushauri kuhusu shughuli za usajili wa biashara;
Kuchambua taarifa za biashara na masoko na ushauri ipasavyo;
Kukuza ubia wa sekta binafsi ya umma;
Kusimamia shughuli za minada na masoko katika Halmashauri;
Kukusanya na kusambaza taarifa za masoko ya bidhaa na huduma kwa wahusika;
Kutekeleza mkakati wa kukuza biashara kwa wachuuzi wadogo na watoa huduma za biashara ndogo ndogo; na
Kuweka mazingira bora ya biashara
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa