Halmashauri ya wilaya ya Songea ni moja ya Halmashauri nane(8) za mkoa wa Ruvuma ziliyoainishwa chini ya sheria ya uwazishaji wa mamlaka za Serikali za mitaa mwa 1982.Ilianza kufanya kazi tarehe 01/01/1982.
Jina Songea lilitokana na jina la Kiongozi wa jadi wa kabila la wangoni chifu Songea. Makaoo makuu yake yapo kata ya Peramiho kijiji cha Lundusi
Asilimia 99.21 ya ardhi ni nzuri kwa shughuli za kilimo, ufugaji na uchimbaji wa madini. Asilimia 0.79 ni eneo la maji ambalo linafaa kwa shughuli za uvuvi.
Kijografia wilaya imepakana na wilaya ya Mbinga , Halimashauri ya manispaa ya Songea kwa upande wa magharibi upande wa kaskazini magharibi imepakana na wilaya ya Nyasa na nchi ya Msumbiji kwa upande wa kaskazini. Hali ya hewa ni mchanganyiko.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa