Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea, wakishirikiana na Kampuni ya Aviv leo Novemba 17, 2025 wameanza ziara katika Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha, lengo ikiwa kujengeana uelewa kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusiana na zao la Kahawa.
Katika ziara hiyo, Watatembelea Halmashauri ya wilaya ya Moshi, Halmashauri ya Wilay ya Arusha, Arusha Jiji pamoja na Halmashauri ya Wilay ya Karatu. Lengo la ziara hiyo ni pamoja na kuangalia changamoto zinazowakumba Wakulima wa Kahawa, lakini ukusanyaji wa ushuru katika zao hilo
Katika ziara hiyo, kwa niaba ya Halmashuri ya Wilaya ya Songea, Mkurugenzi Mtendaji Bi Elizabeth Gumbo, ameambatana na Wataalamu kutoka Idara mbalimbali kutoka Halmashauri kama vile; Fedha, Mapato, Sheria, Kilimo pamoja na Mipango.
Zao la kahawa ni miongozi mwa zao muhim katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, hivyo kwa ziara hii, itasaidia namna sahihi ya kuweka nguvu kwenye mambo muhimu yatayowezesha kukua kwa zao la kahawa.
Maeneo ambayo wataalam hao watatembelea ni pamoja na Bodi ya Kahawa, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Arusha pamoja na Karatu ambao wote ni wakulima wazuri wa zao la Kahawa. Mapokezi katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi yalikua mazuri sana yaliyopelekea yaliyopelekea yenye tija
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa