Katibu Tawala, Mkoa wa Ruvuma Bw. Hassan Bendeyeko akiwasilisha taarifa ya utendaji kuhusu mkoa wake wakati wa mkutano kazi uliowahusisha watendaji wa mkoa wa Ruvuma na Ofisi ya Rais - Utumishi wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ngimba akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) ya kuhimiza uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma mkoani Ruvuma wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.
Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za mkoa wa Ruvuma wakijitambulisha wakati wa mkutano kazi uliowakutanisha na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017 mkoani Ruvuma.
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Thadei Kimati akifafanua kuhusu taratibu zinazohusu masuala ya kiutumishi kwa Watendaji na watumishi wa umma mkoani Ruvuma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.
Sehemu ya watendaji wa Serikali mkoani Ruvuma wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuhusu uwajibikaji katika Utumishi wa Umma , iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ngimba mkoani Ruvuma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa