MKUU wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Wilman Kapenjama Ndile ametembelea na kukagua miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Katika ukaguzi huo aliongozana na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Neema Maghembe, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Simon Kapinga na timu ya wataalamu.
DC Ndile amekagua ujenzi wa soko Peramiho ambalo linatekelezwa kwa fedha kutoka kwenye mfuko wa TASAF ambapo hadi kukamilika kwake kutagharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 200,713,278.57
Vilevile amekagua mradi wa karakana ya jamii ya kutengeneza bidhaa za mbao kama madawati, meza na milango iliyopo katika Kata ya Parangu ambayo imegharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 38,580,000 na Halmashauri ilitoa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana hao fedha kiasi cha shilingi milioni 8 kwa vijana hao kwaajili ya kununua vifaa visivyokuwepo.
Aidha, mradi huu umesaidia kuongeza ajira kwa vijana na kuongeza mapato ya Halmashauri na Serikali kwa ujumla kutokana na biashara ya bidhaa za mbao.
Akizungumza Mheshimiwa Ndile amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii na waendelee kutengeneza bidhaa zenye ubora na viwango vya juu ili waweze kuaminiwa Zaidi na kupewa kazi nyingi ambazo zitawasaidia kupata fedha.
Pia DC Ndile amekagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mpitimbi ambapo walipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 40 kutoka serikali kuu kwaajili ya kutekeleza mradi huu, mradi umekamilika na umeanza kutumika na wanafuzi wa kidato cha kwanza wa mwaka 2023.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa