WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na uratibu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama ameanza ziara ya kikazi katika Jimbo la Peramiho.
Ziara hiyo imeanza Jana tarehe 9 Julai 2023 ambapo aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Neema Maghembe, Viongozi wa Chama, Waheshimiwa Madiwani pamoja na timu ya Wataalamu ambapo alitembelea Kata ya Ndongosi.
Akizungumza katika ziara hiyo amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Pia Mheshimiwa Jenista amemshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukuza uchumi kwa Wananchi hususani wakulima kwa kuwasongezea huduma za ruzuku karibu na maeneo yao na kwa bei nafuu, hivyo amewataka wananchi kutumia fursa ya kilimo vizuri ili kukuza uchumi.
“Pamoja mnajishughulisha na shughuli za kilimo pia endeleeni kubuni vyanzo vingine vya kuingiza mapato kwani Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala la maendeleo ya wananchi imejipanga vizuri ili kuhakikisha wananchi wanapata maisha bora na salama”, amesisitiza Mhe. Jenista.
Aidha, Mheshimiwa Jenista amewataka Wananchi kuacha tabia za kukata miti ovyo katika maeneo yao na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji kwani huo ni uharibifu wa mazingira unaosababisha kukosekana kwa maji.
Vilevile Mheshimiwa Jenista amewaasa vijana kutojishughulisha na shughuli za kilimo cha bangi na matumizi ya madawa ya kulevya kwani inaleta athari kubwa katika Afya ya akili.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa