MKUU wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile amewataka Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji waweke utaratibu wa kusikiliza na kutatua kero za migogoro ya ardhi katika maeneo yao.
Ametoa kauli hiyo jana Juni 28, 2023 katika mkutano wa adhara uliofanyika katika Kata ya Muhukuru Kijiji cha Nakawale ambapo lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kijiji hicho.
Katika ziara yake aliambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji, kamati ya ulinzi na usalama Wilaya pamoja na timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Akizungumza katika mkutano huo amewataka wananchi wote ambao wameuza ardhi za Kijiji pasipo kufuata taratibu na sheria warejeshe ardhi hizo katika Serikali ya Kijiji.
‘‘Ardhi ni mali ya Kijiji kitendo cha kuuza ardhi ni ulanguzi unaotokana na tamaa hivyo unawanyima haki vizazi vinavyokuja sasa watu wote mliouziana ardhi bila kufuata taratibu huo ni ubatili hizo ardhi zitarejeshwa katika Serikali ya Kijiji’’, amesisitiza Mhe. Ndile.
Aidha, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa katika Kijiji cha Nakawale Serikali ya Kijiji haijawahi kutenga eneo la ufugaji ni eneo la kilimo hivyo kama kuna wafugaji wameingiza mifugo katika eneo hilo waiondoe.
Vilevile amesema ardhi ya Tanzania haiuzwi bali inamilikishwa kutoka kwa mtu mmoja Kwenda kwa mwingine hivyo kwa mwananchi yeyote anaetaka kumiliki ardhi ahakikishe anapeleka maombi katika ofisi ya Serikali ya Kijiji ili maombi yake yaweze kujadiliwa na sio kitendo cha kumilikishana bila kufuata taratibu.
Pia katika mkutano huo uliambatana na zoezi la kuunda tume yenye watu 11 kutoka katika kila Kitongoji kwa kushirikiana na wataalamu wa ardhi kutoka Halmashauri kufanya uchunguzi wa kina na kitaalamu wa migodoro hiyo na majibu kutolewa kwa muda watakaopewa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa