KAMATI ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea imeendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Songea Vijijini.
Kamati hiyo iliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Simon Kapinga ilianza kukagua mradi wa SWASH ujenzi wa matundu 13 ya vyoo katika shule ya msingi Makambi uliotekelezwa kwa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 34.2
Pia Kamati ilitembelea na kukagua ujenzi wa vyoo matundu 14 mradi wa SWASH ambao unatekelezwa kwa fedha kiasi cha shilingi Milioni 34.2
Vilevile ilitembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa BOOST wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo unaotekelezwa kwa kiasi cha shilingi Milioni 53.1
Wakisoma taarifa Walimu wakuu wa shule ambazo zimetembelewa wametoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Joakim Mhagama kwa kuendelea kuwapigania na kuwaletea fedha za miradi ya maendeleo.
Pia wametoa shukrani kwa Baraza la Madiwani, Viongozi wa Chama pamoja na timu ya Wataalamu kwa usimamizi wa karibu wa miradi hiyo.
Akizungumza Makamu Mwenyekiti Mhe. Kapinga amewasisitiza wananchi wanapoletewa fedha kwa ajili ya miradi wajitahidi kutoa ushirikiano wa kutosha pale zinapohitajika nguvu za Wananchi ili fedha ziweze kutumika kununulia vifaa vya viwandani na miradi iweze kukamilika kwa wakati na viwango vinavyokubaliwa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa