Wakazi wa Peramiho Wameanza Kunufaika na Stend ya Kisasa ambayo imezinduliwa Leo Julai Mosi 2025 na Kanali Ahmed Abbas Ahmed Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mradi wa Ujenzi wa Stend ya Kisasa Umetekelezwa kwa Kutumia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Tanzania Social Action Fund awamu ya Tatu Kwa Kushirikiana na Wananchi wa Kijiji Cha Lundusi, Zaidi ya Milioni 600 Zimetumika Kutekeleza Mradi huo.
Mkuu. wa Mkoa wa Ruvuma akizindua Stend hiyo ya Kisasa amewashukuru sana Watendaji wote wa TASAF, kwa Kazi nzuri Waliyoifanya kwa Kushirikiana na Wananchi Kuhakikisha Stend hiyo inakamilika ikiwa na Miundombinu yote Muhimu, nakuwataka Wananchi wa Peramiho Kumpatia Heshima anayostahili aliyekuwa Mbunge wa Jimbo Hilo ambaye pia ni Waziri wa Afya Jenista Mhagama kwa Kupambania Upatikanaji wa Stend hiyo ya Kisasa akishirikiana bega kwa bega na Halmashauri ya Songea DC, akimshukuru pia Dkt.Samia Kwa kutoa Fedha nyingi za Miradi Mkoani Ruvuma,pamoja nakuwashukuru Wananchi.
RC Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakiwemo Wananchi wa Peramiho Kuitunza nakuilinda Miundombinu hiyo ya Stend, ili waendelee kupata Huduma iliyobora ya Usafiri Katika Mazingira Rafiki, Nakuwaagiza Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile na Mkurugenzi Mtendaji wa Songea DC Bi. Elizabeth Gumbo kuhakikisha kunakuwa na Miundombinu ya Maji ya Uhakika kwa ajili ya Huduma ya Vyooni na Matumizi ya Maji kwa abiria, Madereva na Watu Wote ambao Watatumia Stend hiyo ya Kisasa iliyosheheni Maduka , Ujenzi wa Ofisi, Ujenzi wa Uzio.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Kutoka Makao Makuu Bwn. Shadrack Mziray ameishukuru Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyopambania Watu kuondokana na Umaskini Kupitia Miradi Mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo TASAF Kuwezesha Kaya Maskini katika Kuwaongezea Kipato na Fursa anuai za Kiuchumi, na tangu kuanzishwa kwa TASAF Mwaka 2000 Hadi kufikia sasa Zaidi ya Shilingi Trillion 1 Kama Ruzuku zimewafikia Walengwa hapa Nchini, akibainisha kwamba ifikapo Septemba 30 Mwaka huu Mradi huo Utahitimishwa Kote Nchini, ambapo Walengwa ambao hawajapokea Malipo Yao Watalipwa Kabla ya Mwezi Sept, Lakini Mradi Mwingine Mpya Utaanza Mwezi Octoba Mwaka huu.
Wananchi wenyewe wanasema Ujenzi wa Stend ya Kisasa Peramiho Utawapunguzia aghali ya Usafiri, Wananchi wa Lundusi na Wale waishio Maeneo Jirani Hutumia Shilingi 1500 Hadi 2000 Kutoka Hospital ya Mtakatifu Joseph Peramiho Hadi Kufika Kijiji Cha Lundusi na Zilipo Ofisi za Halmashauri ya Songea DC, Ikilinganishwa na Nauli ya 1200 Kutoka Songea Mjini Hadi Kufika Peramiho, Wameishukuru sana TASAF na Serikali ya Dkt. Samia, Wakimpa Heko na Jenista Mhagama Waziri wa Afya na Mbunge aliyemaliza muda wake.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa