Wizara ya Maliasilia na Utalii imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kutaka somo la historia ya Tanzania lifundishwe kwenye shule.
Hayo ameyasema waziri wa maliasili na utalii Dkt Damas Ndumbaro wakati akifungua tamasha la 12 la kumbukuzi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa ndani lililofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Manispaa ya Songea leo.
“Kupitia Makumbusho ya Taifa tunaunga mkono na kutekeleza agizo la Rais la kufundisha somo la historia ya Tanzania”,amesema Dkt Ndumbaro.
Dkt Ndumbaro amesema katika kutekeleza agizo la Rais Dkt Magufuli Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya kielimu ya Makumbusho imezindua klabu sita za historia na uzalendo kwenye shule kwa lengo la kukuza ufahamu wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuhusu historia ya nchi yetu.
Dkt Ndumbaro amesema Makumbusho ya Taifa ni Taasisi ya Kielimu yenye jujkumu la kukusanya ,kutafiti, kuhifadhi na kuelimisha jamii kuhusu urithi wa Taifa letu,hivyo lina wajibu mkubwa katika kufundisha jamii historia ya Tanzania kwa vitendo yakiwemo matamasha na utalii wa kiutamaduni.
Kwa upande wake Dkt Christowaja Ntandu ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa michache inayo tekeleza kwa vitendo matamasha ya kiutamaduni na kukuza utalii wa ndani wa malikale .
Ntandu amesema tamasha la kumbukizi ya vita vya majimaji na utalii wa utamaduni limekuwa linaumuhimu mkubwa kwasababu linatoa elimu kwa Watanzani kupitia makongamano na semina kuwafundisha Watanzania kujenga uzalendo, mshikamano,upendo na kupenda vya kwetu.
Ameongeza kwakusema tamasha linatoa fursa ya pamoja ya kutafakari,kuenzi na kusherehekea matunda ya uzalendo ya wazee wetu ambao ni mashujaa wa vita vya majimaji ambao walipambana katika kuupinga utawala wa kikoloni mwaka1905 hadi 1907.
Tamasha la kumbukizi ya Vita vya majimaji ni la 12 tangu lianzishwe mwaka 2010 na miaka 114 imepita tangu mashuja hao wa vita kunyogwa katika eneo la Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma likiwa linaandaliwa na Baraza la wazee wa mila na desturi,jeshi la wananchi na makumbusho ya Taifa.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa habari Songea dc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa