Naibu Waziri wa kilimo David Ernest Silinde amesema Wizara ya kilimo itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuleta tija katika kilimo cha kahawa wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kahawa Songea uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea 06 Disemba 2023.
Pamoja na mambo mengineMhe Naibu Waziri amesema zao la kahawa ni miongoni mwa mazao ya kimkakati nchini Tanzania ambalo linaliingizia fedha nyingi za kigeni hivyo Wizara ya kilimo imejipanga kikamilifu kusimamia vyema zao hilo. Amesema
“ Niseme kwamba Wizara ya kilimo tumejipanga vizuri hata kwenye zao hili la kahawa nyinyi nyote mnafahamu, zao la kahawa ni ,moja ya mazao ya kimkakati ya kibiashara tuliyonayo nchini ukiacha korosho, tumbaku, pamba na katani zao la kahawa ni miongoni mwa ,mazao makubwa nchini ambayo sisi kama Wizara tunalitegemea na ni zao ambalo linaingiza fedha nyingi za kigeni katika nchi yetu, kwahiyo niwaondoe shaka maamuzi na ubunifu ambao Mkuu wa Wilaya umeuleta kwa wananchi wako wa Halmashauri zako ni uamuzi unaoonekana unalengo la ilani ya chama cha mapinduzi kuhakikisha kwamba tunawainua wananchi lakini mkakati wetu wa kufufua haya mazao ya kibiashara tunautekeleza kwa vitendo kwahiyo katika hili mimi nikushukuru na niwaahidi tu Wizara ya kilimo itaendelea kutoa ushirikiano”
“ Lakini kipekee naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mhe Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wizara ya kilimo, nadhani tunaona sasa hakuna changamoto ya upatiukanaji wa mbolea kwani anatoa mbolea za ruzuku kwa kila mkulima , pia namshukuru Waziri wa kilimo Mhe. Hussein Bashe kwa kuipambania wizara hii ya kilimo, pia shukrani zimuendee Mkuu wa Mkoa wa Ruvua Kanal Laban Thomas kwa mapokezi yake mazuri na kutupa kibaria cha kufanya mkutano huu, pia nakushukuru Mkuu wa Wilaya ya Songea Kwa maandalizi ya Mkutano huu na Wadau wote wa Kilimo cha kahawa ambao nyinyi ndio mliotufanya sisi tuwepo mahali hapa.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile amewataka wakulima kuacha kutegemea kilimo cha zao moja badala yake waongeze na kilimo cha kahawa kwani ni kilimo chenye tija hivyo kitawawezesha kuepukana na umasikini. Amesema
“ Tanzania inamazao mengi ya kimkakati ikiwemo kahawa, kwanini tunasema ni zao la kimkakati kwasababu linaingizia fedha za kigeni taifa hili na kwa kufanya hivyo linapunguza umasikini kwa Watanzania, hivyo Wilaya ya Songea ni moja ya Wilaya iliyobahatika kuwa na hali ya hewa nzuri , udongo mzuri wenye rutuba na maji ya kutosha ambayo yanachochea uzalishaji wa zao la kahawa, hivyo ndugu zangu waku;lima tuamke sasa na kuchangamkia fursa hii na tunatakiwa tubadilike tuachane na kilimo cha msimu kwani kahawa unaweza kupanda mwaka huu lakini ukawa unavuna mpaka unazeeka.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa zao la kahawa wilaya ya songea katika mkutano wa wadau wa kahawa songea Frank Sungau amesema “ uzalishaji wa kahawa kwa msimu wa mwaka 2020/2021 wilaya ya songea ilizalisha jumla ya Tani 1,888.43, mwaka 2021/2022 ilizalisha Tani 2,016.3 na mwaka 2022/2023 ilizalisha tani 3,040.89 ambapo mapato ya halmashauri yatokanayo na zao la kahawa ni , kwa 2020-2023 Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni 888,042,443.58, kwa Halmashauri ya Madaba ni 2,341,420.00 na Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni 842,500.00”.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa