Mwekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Mh.Menasi Komba amewaagiza wenyeviti wa Vijiji kushiriki na kusimamia kwa uadilifu kazi ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri .
Komba ametoa agizo hilo katika kikao cha kawaida cha mwenyekiti wa Halmashauri na wenyeviti hao kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Komba amewaagiza wenyeviti wa Vijiji kushiriki na kusimamia kwa uadilifu kazi ya ukusanyaji mapato na kuto kujihusisha na hujuma yoyote katika kazi hiyo na atakaye bainika hatasita kumchukulia hatua za kinidhamu.
Amewaagiza kuwafuatilia na kuwa tambua wakulima na wafugaji wakubwa katika Vijiji vyao kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya utoroshaji wa mapato ya Halmashauri.
Kwaupande wake kaimu mweka hazina wa Halmashuri hiyo Yasini Mohamedi Twaha amesema kitika kazi ya ukusanyaji wa mapato,serkali imeanisha vyanzo ambavyo ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri itahusika kuyasimamia na vyanzo ambavyo vinaweza kukusannywa na mawakala .
Yasini amevitaja vyanzo ambavyo vinasimamiwa na Halmashauri kuwa ni leseni za biashara,ushuru wa huduma,leseni za vileo,kodi ya majengoya biashara,kodi za majengo ambazo awali zilikuwa zilikuwa zikikusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania,vibali vya ujenzi na vingine ni mauzo ya viwanja na upimaji wa ardhi,ada za ukaguzi wa mifugo,ada ya dhabuni, ushuru wa minada na ada na tozo nyingine kwa mujibu wa sheria ya fedha ya serikali za mitaa ya mwaka 1982.
Amevitaja vyanzo vya mapato ambavyo Halmashauri itahusika kuwapa wakala ni ushuru wa madini ya ujenzi,maegesho ya magari,ushuru wa soko,ushuru wa mazao na ushuru wa mazao ya misitu.
Ameongeza kwakusema kwa mujibu wa mwongozo mpya wa ukusanyaji mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wakala atalipwa asilimia 10 ya makusanyo aliyoyawasilisha.
Baadhi ya wenyeviti wametoa ushauri kuwepo na kikosi cha doria ambacho kitakuwa shirikishi katika kukabiliana na baadhi ya wafanyabiashara na wafugaji wasumbufu katika kulipa ushuru pamoja na kutokuwapa wakala mkataba wa muda mrefu kwalengo la kuepusha kuzalisha madeni .
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery,
Afisa Habari Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa