Madaktari Bingwa Zaidi ya saba, wanategemea kuwepo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kuanzia Mei 26, 2025 hadi Meji 31, 2025 kwa lengo la kutoa huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi kwa Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Akilizungumzia hili, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bi Elizabeth Mathias Gumbo, Amewatangazia wananchi wote kuwa kuanzaia Tarehe 26-31 Mei 2025, kutakua na huduma za kibingwa na Ubingwa Bobezi katika hospitari ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.“ MADAKTARI WA RAIS SAMIA “ambao watakuwepo kuhudumia Wananchi wote katika Hospitari ya Wilaya.
Lengola Ujio wa Madaktari Bingwa ni muendeleza wa mapenzi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wake katika kuimalisha ubora wa matibabu na kupunguza vifo kwa makundi mbalimbali hasa vinavyotokana na uzazi na Watoto wachanga.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Dr. Geofrey Kihaule amesema “ katika Hospitari ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea tunategemea kupokea seti ya madaktari saba, (7) ambao watajikita kutibu magonjwa kwa wagonjwa mbalimbali, huku akitaja Madaktari watakaokuwepo na Magonjwa yatakayoshughulikiwa kama vile:-
Daktari Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemaanisha hasa kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora ya Afya, na pia kuhakikisha anawaleta madaktari Bingwa mala kwa mala ikiwa ni Sehemu ya kuwapunguzia wananchi kero ya kusafili kuelekea muhimbili kupata huduma.
Kwa niaba ya Mkurugenzi, Dr. Kihaule amemshkuru sana Dkt Samia, na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, kwa kuendelea kuhakikisha Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, wanapata Huduma bora ya Afya.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa