Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Robo ya tatu yaani Januari- Machi, 2024/2025 uli0fanyika leo april 19, 2025 ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea – Lundusi ambao Umeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhe. Simon Kapinga, Huku Katibu wake akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi Elizabeth Mathias Gumbo, wamemshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Waziri wa Afya ambaye pia ndio Mbunge wa Jimbo la Peramiho kwa mambo makuu walioifanyia Songea DC.
Akizungumza katika Mkutano huo kwa niaba ya Madiwani, Mhe Kapinga amesema “Tunamshukuru sana Mhe Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kila kata iliyopo halmashauri ya Songea kupata Fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, Amemshukuru Pia Mbunge kwa kuwaletea wananchi wa jimbo la Peramiho maendeleo, na hasa Kuleta Madaktari Bingwa kwa ajili ya Kuwatibu wananchi wa Songea.
Mkurugenzi Mtendaji Bi Elizabeth Gumbo, alitumia fursa hiyo ya Baraza pia kuwaarika viongozi wote na Wananchi katika Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, unaotegemea kufika katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mei 10, 2025.
“Mweenge Wetu wa Uhuru utaingia Halmashauri yetu kupitia Kata ya Mpandangindo na utapitia miradi yetu kisha kutakua na mkesha katika kata ya Magagura. Hivyo naomba wageni wote mliohudhulia kikao hiki, tuungane pamoja kuhakikisha tunakesha pamoja na Mwenge” Gumbo
Mkutano huo uliobeba Agenda 10, pamoja na mambo mengine kulikua na uwasilishaji wa taarifa kutoka kwenye kamati mbalimbali kama vile, Kamati ya Maadili, kamati ya kudhibiti Ukimwi, Kamati ya Elimu Afya na Maji, Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa