Mkutano Maalumu wa Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri ( Mawasiliano Serikalini) uliofanyika jijin Dodoma katika Mji wa Kiserikali Mtumba, ulioanza Mei 23, 2025 na Kumalizima Mei 24,2025 Ulifunguliwa na Mhe Mohamed Mchengerwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Kufungwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Msigwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mkutano huo umemalizika huku ukiwa na mtazamo wa pamoja ulio chanya kwa maslahi mapana ya Nchi.
Mkutano huo uliokua na lengo la kukumbushana majukumu, lakini pia kushauliana mambo mbalimbali ya kiutendaji pamoja na kujadili changamoto zinazowakuta Wanahabari katika kutimiza majukum yao.
Viongozi hao, Pamoja na mambo mengine wameendelea kusisitiza juu ya wanahabari kuwa Wazalendo katika kuipigania Nchi yao huku wakisisitizwa kuwa kama wanahabari wote watatimiza majukumu yao vema, wananchi watayaona na kuyasikia mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Haasan.
“Hakikisheni mnaandika habari zenye hamasa na kuibua ushuhuda kuhusu kazi za serikali nan a miradi inayotekelezwa ambapo viongozi wa ngazi husika na wananchi wa wakaida wahusishwe kuusemea mradi au kazi Fulani zinazotekelezwa katika maeneo yao” Mhe Mchengerwa
Ameelekeza pia Maafisa Habari washiriki ziara za viongozi na Timu za ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo na kupatiwa mafunzo mbalimbali yanaendana na taaluma zao, huku akisisitiza kuwapatia stahiki zao ili kuwezesha utendaji wa kazi zao.
“Maafisa habari mnapaswa kuwa sauti ya serikali katika maeneo yenu, mnawajibu wa kuhakikisha mafanikio ya serikaliyanawafikia wananchi na pia changamoto zinazojitokeza zinaelezwa kwa uhalisia wake” Msigwa
Maafisa habari, baada ya kupokea maelekezo ikiwa ni pamoja na kuhakikishiwa kufatiliwa na kuwekwa sawa kwa mambo yao ikiwa ni pamoja na Ofisi, Vitendea kazi na maslahi yao, wameahidi kuendelea kuisemea serikali kwa mambo mazuri yanayofanywa katika uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa