• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

WENYEVITI wa vyama vya msingi vya Ushirika Songea waonywa

Tarehe ya Kuwekwa: April 9th, 2021

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Mhe. Menas Komba amewaonya Wenyeviti wa Vyama vya Msingi vya Ushirika na wadau wa ushirika kujiepusha na udanganifu wa kuiba mazao ya wakulima kwa njia ya kuchezea mizani.

Mhe. Komba ametoa onyo hilo katika kikao cha viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika na wataalamu wa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri hiyo kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo mji mdogo wa Peramiho.

 Mhe. Komba amesema kumekuwa na malalmiko mengi toka kwa wakulima wakiwalalamikia viongozi na wadau wa Ushirika kuwaibia mazao yao kwanjia za ujanja ujanja kwakuchezesha mizani kwania mbaya ya kuwadhurumu haki yao.

“Sipendi kusikia malalamiko toka kwa wakulima,kuibiwa mazao kupitia vipimo”,amesema Mhe. komba.

Mhe. Komba amesema Ushirika uliundwa kwa lengo la kusimamia shughuri za wakulima na kuwasaidia hivyo viongozi na wadau wa ushirika wanatakiwa kuwa makini katika kuwahudumia wakulima na kutambua mkulima ndio mtaji mkubwa wa ushirika pasipo mkulima hakuna ushirika.

Mhe. Komba amewaagiza viongozi wa Ushirika wa Halmashauri hiyo kushiriki kikamilifu katika zoezi la kudhibiti utoroshaji wa mazao toka ndani ya Halmashauri kwenda Halmashauri nyingine kwasababu kitendo hicho kinaikosesha Halmashauri mapato yanayotokana na ushuru wa mazao baada ya kutoroshwa.

Ameongeza kwakusema Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni Halmashauri yenye rasilimali za kutosha kama vile mito inayotiririsha maji kipindi chote cha mwaka,eneo kubwa linalofaa kwashughuri za kilimo,mvua za  kutosha na shehena ya madini ya makaa ya mawe, kinachohitajika ni ushirikiano katika usimamizi na ufuatiliaji  kwenye eneo la ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wao viongozi wa vyama hivyo wamesema kutokuwepo kwa bei elekezi ni changamoto kwao kwasababu Makampuni yanakuwa huru kupanga bei wanazozitaka jambo linaoneka kumnyonya mkulima.

Wamesema msimu wa kilimo wa mwaka 2020 /2021 hapakuwa na bei elekezi badala yake Wizara ya Kilimo Ushirika na Umwagiliaji iliagiza mazao yatauzwa kulingana bei ya soko ya siku husika kitendo ambacho kiliwasikitisha wakulima.

Naye Meneja wa Chama kikuu cha Ushirika cha SONAMCU Juma Mwanga ametoa wito kwa wakulima kuzingatia usafi wanapoandaa mazao yao kwa nia ya kuyafikisha sokoni kwa vile makampuni yanayonunua mazao ya wakulima yamekuwa yakifanyabiashara maeneo mengine, mazao yakiwa machafu yanakosa sifa kwamnunuzi.

 Mwanga ametoa rai kwa viongozi hao kuonyesha moyo wa uzalendo na kudumisha mshikamano kwakurudisha fadhira kwa wanachama kwenye makazi yao kwakuchangia ujenzi na utekelezaji wa miradi ya kijamii mara wanapolipwa ushuru wao.

Afisa ushirika wa Halmashauri hiyo Damian Lwena amesema ushirika ni nyenzo muhimu sana katika kufanikisha malengo ya wakulima,viongozi wasimamie vema ushirika na kuacha tabia za ubadhirifu wa mali za chama.

 Lwena amesema kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2021 /2022 wanakadiria kuvuna tani 3,304 za mazao yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi gharani ambayo ni ufuta tani 2678, soya tani 473 na mbaazi tani 253.

Halmashauri ya Wilaya ya Songea inajumla ya vyama vya msingi vya ushirika 16 ambavyo vimesajiliwa na vinafanyakazi kwa mujibu wa kanuni,taratibu,na Sheria za nchi.

Imeandikwa na

Jacquelen Clavery

A/habari Songea dc

9/04/2021.

 

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • FAHAMU KUHUSU BARAZA LA MADIWANI; MUUNDO NA UTENDAJIKAZI WAKE

    November 25, 2025
  • SONGEA DC, YATEMBELEA MIKOA INAYOLIMA KAHAWA KWA LENGO LA KUPATA UZOEFU

    November 19, 2025
  • DC NDILE AIPONGEZA HALMASHAURI YA SONGEA KWA KUIMARISHA HALI YA LISHE, ATOA WITO WA KUENDELEZA JITIHADA

    November 17, 2025
  • SONGEA DC YAPOKEA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA TSH MILIONI 30 KITUO CHA AFYA MUHUKURU LILAHI

    November 20, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa