WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma na Utawala bora Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama amewaagiza Maafisa Utumishi kuwa wasimamizi wa maadili, nidhamu, wajibu, na haki za watumishi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea katika ukumbi wa mkutano wa Jimbo la Peramiho uliopo katika Ofisi ya Mkurugenzi Songea .
Akizungumza katika Halmashauri hiyo Mheshimiwa Waziri Jenista ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuweza kushika nafasi ya tano kitaifa kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani.
‘’Ninawaomba Maafisa Utumishi msimamie vyema mpango wa mafunzo hasa kwa kuzingatia mahitaji ya Ofisi Pamoja na kusimamia semina elekezi kwa ajira mpya zote’’, amesisitiza Mheshimiwa Jenista.
Hata hivyo ameziagiza mamlaka za ajira na Maafisa Utumishi wasimamie mazingira bora ya kazi ili kupunguza uhitaji wa kuhamahama kwa watumishi hao.
Mheshimiwa Waziri Jenista ameongeza kuwa Maafisa Utumishi kuwa na vikao vya mara kwa mara na watumishi ili kutatua changamoto zinazowakabili na kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Menace Komba ameahidi maagizo yote yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri kuyafanyia kazi kwa weledi ili kuhakikisha Halmashauri hiyo inasonga mbele kwa Maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa