Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro amefuta vibali vyote vya uchomaji mkaa katika Vijiji vya Mbangamawe,Hangangadinda na Nderenyuma katika Kitongoji cha Kilimahewa maarufu kwa jina la“slow”katika Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma kufuatia mgogoro wa wananchi na askari wa maliasili na wauhifadhi.
“Haiwezekani kuendelea kukata miti kuanzia leo vibali vyote vya mkaa vinakwisha”amesisitiza Dkt Ndumbaro.
Dkt Ndumbaro amefuta vibali hivyo kufuatia malalamiko na mgogoro unaodaiwa na wananchi wa Vijiji hivyo kuvamiwa na askari wa maliasili na wauhifadhi kuwataka waondoke kwenye makazi yao ambayo ni mapito ya asili ya wanyama pori kwa kuwachomea moto vibanda vyao na kuwapora mali zao mnamo Machi 5 na 6,2021.
Kufuatia malalamiko hayo Dkt Ndumbaro amefika katika Kijiji cha Mbangamwe na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi pia kuhaidi kuunda tume itakayo washirikisha viongozi wa CCM ya kuchunguza madai ya malalamiko hayo kwa lengo la kubaini ukweli na uongo endapo kweli utabainika wahusika wote watachukuliwa hatua za kisheria pasipo kumwonea mtu
Dkt Ndumbaro amesema wananchi hawatanyang’nywa maeneo yao wanayo yamiliki bali wataendelea kuyamiliki ,nje na makazi kwenye mashamba yao wataruhusiwa kufanya shughuli zinazo kwenda sambamba na uhifadhi na utalii.
Dkt Ndumbaro amezitaja kazi ambazo wananchi wanatakiwa kufanya kwenye mashamba wanayo yamiliki kuwa ni upandaji wa miti ya kibiashara na ufugaji wa nyuki tu.
Dkt Ndumbaro amesema Wizara yake kupitia watalam wake wa Maliasili na Utalii watakwenda katika Vijiji hivyo kutoa elimu ya ufugaji nyuki na upandaji miti na kugawa mizinga kwa ajili ya kufugia nyuki bure kwenye vikundi vyote vilivyo sajiliwa.
Dkt Ndumalo amesema maeneo yote ya uhifadhi yanatakiwa kulindwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya Watanzania wote, hivyo wananchi waliouziwa maeneo kwenye hifadhi wafikirie kufanyakazi ya uhifadhi na sio vinginevyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amewatupia lawama viongozi wa Vijiji na Watendaji wake kwa kukiuka maagizo ya Serikali ya kuuza ardhi kiholela bila kufuata utaratibu na kuzalisha migogoro na malalamiko katika jamii.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho ametoa wito kwa wananchi kuzingatia miongozo na maelekezo yanayotelewa na viongizi wa Serikali katika swala zima la kulinda na kutunza maliasili.
Amesema wananchi watakuwepo na ushoroba utakuwepo hivyo ni jukumu la viongozi kuwaelimisha wananchi kuhusu muhimu wa uwepo wa maeneo ya uhifadhi na utalii katika makazi yao kitendo ambacho kitasaidia kuepusha purukushani baina yao na Serikali.
Historia inaonyesha kwamba katika kipindi cha miaka kati ya 1970 hadi 1986 katika maeneo ya Vijiji hivyo Wanyama pori walikuwa wakiishi na wakipita njia kuelekea upande wa pwani ya Msumbiji na kurejea Tanznia na vijiji hivyo vilikuwa bado havijasajiliwa.
Imeandaliwa na kuandikw na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari Songea dc
24,04,2021
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa