Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (MUUUB) Jusseim Mwakipesile amewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili katika utumishi wao na kutambua madhara ya ukiukwaji wa maadili.
Mwakipesile ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo ya maadili na ushughulikiaji wa malalamiko ya wananchi katika utumishi wa umma yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea katika mji mdogo wa Peramiho.
Mwakipesile amesema Watumishi wa umma katika utumishi wao wa kila siku wanatakiwa kuzingatia maadili na ukiukwaji wa maadili ni matokeo hasi katika kufikisha huduma kwa wananchi pamoja na kuleta madhara ya kuzalisha wataalam wasio na viwango vinavyotakiwa,matumizi mabaya ya rasilimali za nchi na vifo vinanavyotokana na sababu hiyo.
Mwakipisele ametaja baadhi ya madhara yanayotokana na ukiukwaji wa maadili ni pamoja na ufisadi,uroho na ubinafsi,unyapara mahala pakazi unao fanywa na baadhi ya vionngozi,usiri wa umiliki mali ,mgongano wa maslahi na udanganyifu.
“Watumishi wote wanafanyakazi kwa niaba ya Rais,na Rais ndiyo msimamizi wa maadili kutozingztia maadili ni kuidharirisha Serikali”
Aidha amewataka viongozi na wakuu wa idara kusoma katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,miongozo, na kanuni mbali mbali za utumishi wa umma ili wanapofanya maamuzi juu ya jambo wawena uhakika na wanachokifanya pasipo toa upendeleo au kumwonea mtu.
Kwa upande wake Afisa Habari mwandamizi wa OR-MUUUB Rocky Setembo amesema umuhimu wa kushughulikia malalamiko kwa ufanisi sehemu ya kazi utaimarisha usikikivu,uwajibikaji wa utumishi na utaboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Ametaja vyanzo vya malalamiko kuwa ni taratibu zinazo kinzana zilizoko katika sheria,kanuni na miongozo,taarifa kukosa taarifa sahihi au kutopata kabisa,watumishi kutoa majibu ya kukutisha tamaa yanayopelekea wateja kujenga dhana potofu,vifaa kutokidhi mahitaji ua kutokuwepo,wateja kutozingatia utaratibu uliowekwa,umri ,wivu mila na desturi.
Imeandikwa na,
Jacquelen Clavery.
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa