Watumishi
Halmashauri ya Wilaya ya Songea inaupungufu wa watumishi 294 wa idara ya Afya kati ya 472 wanaotakiwa kwa ikama
Hayo ni kwa mujimu wa mganga mkuu wa Halmashauri wilaya ya songea Dr Yeseya Mwasubira.
Dr Mwasubira amesema idara ya Afya inaupungufu wa watumishi 294 na waliopo ni watumishi 178 wakiwemo walioajira hivi karibu, na kwa ikama wanatakiwa jumala ya watumishi 472.
Aidha amesema Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepokea watumishi 22 kutoka OR TAMISEMI wa ajira mpya wakiwemo Madaktari daraja la II wa 2,Tabibu daraja la II mmoja,Tabibu wasaidizi wa 3,Afisa wauguzi wa saidizi daraja la II wa 5,Wauguzi daraja la II wa 5,Tabibu wasaidizi daraja la II 3 na wengine ni Maafisa uuguzi daraja la II wa 5 Wauguzi wasaidizi daraja la II wa 5 Mfamasia daraja la II mmoja,Afisa Afya Mazingira msaidizi mmoja Watekinolojia dawa daraja la A II wa 2,Mtekinolojia maabara msaidizi mmoja na Muhudumu wa Afya mmoja.
Halmashauri ya Wilaya Songea ina zahanati 31, kituo cha afya kimoja na Hospitali ya Wilaya moja
JACQUELEN CLAVERY -TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa