Watahiniwa 5157, ikijumuisha wavulana 2527 na wasichana 2630 wa darasa la nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, leo Octoba 22, 2025, wameungana na wanafunzi wengine Nchini kukuketi kwa ajili ya mtihani wao wa Taifa
Akizungumza kwa niaba ya Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi. Elizabeth Gumbo amewataka kila la kheri wanafunzi wote wa darasa la nne ndani ya Halmashauri hiyo katika mitihani Yao ya kujipima ya Taifa ambayo Imeanza Leo Oktoba 22 na inatarajiwa kumalizika Octoba 23 2025.
Katika hatua nyingine amewashukuru walimu wa shule zote katika Halmashauri hiyo kwa kuwaandaa vyema wanafunzi hao na kusema anawaombea kwa mwenyezi Mungu ili wafanye mitihani Yao salama kabisa.
Amabapo masomo 6 yatakayokwenda kupimwa ni Sayansi, Hisabati Jiografia na mazingira; Sanaa na Michezo, Kiswahili, English language, Historia na maadili. Pia kuna masomo ya kuchagua ambayo ni France, Arabic, Chinese.
Umuhimu wa upimaji wa kitaifa kwa darasa la 4 ni kuangalia kiwango cha juu cha stadi za juu za kusoma, kuandika na kuhesabu ambapo hupimwa kiwango cha umahiri kwa masomo yanayotahiniwa katika ngazi hio.
Lakini matokeo ya upimaji huu huwawezesha wakuu wa shule na walimu kubaini changamoto za wanafunzi katika mbinu zilizotumika kwenye ufundishaji na ujifunzaji Ili kuboresha mbinu mpya za ufundishaji na ujifunzaji.
Aidha Baraza la mitihani limeendelea kusisitiza kuwa wasimamizi walioteuliwa kufanya kazi hiyo kwa umakini, weledi na uadilifu wa hali ya juu ili kila mwanafunzi apate haki yake ya msingi.
Watahiniwa wote watafanya upimaji huu katika muda uliopangwa. Baraza limewataka wasimamizi wawape watahiniwa haki zao za msingi kulingana na mahitaji yao kama karatasi za nukta nundu kwa wanafunzi wenye uhitaji maalumu na karatasi zilizokuzwa maandishi kwa watahiniwa wenye uoni hafifu.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa