Watawa wafungua daraja
Watawa wa Shirika la Mt Agnes Chipole wamerususu wananchi kutumia daraja la Tulila mto Ruvuma katika kijiji cha Mipeta
Wananchi wameruhusiwa kutumia daraja hilo kufuatia mazungumzo ya pamoja baina ya Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh Pololeti Mgema na uongozi shirika hilo.
Awali wananchi waliruhusiwa kutumia daraja hilo mara baada ya kukamilika kujengwa,lakini baada ya kurusiwa baadhi ya wananchi ambao sio waaninifu walianza kuhujumu miundo mbinu ya darja hilo kwakuiba vifaa mbalimali vilivyotumika kujengea daraja hilo.
Kufuati hali hiyo Shirika la watawa likaamua kuzuia wananchi kupita katika daraja hilo na kuwa jengea daraja sehemu nyingine ambalo limeonakana linaweza kuhatarisha maisha ya wananchi wa kijij cha Mipeta na maeneo mengine.
Mh Mgema ameagiza uwepo ulinzi Shirikishi baina ya wanakijij cha Mipeta na watawa katika kuhakikisha miundo mbinu ya daraja hilo inalindwa na kubaki salama,pia wananchi warusiwe kupita kwa masharti ya muda kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni baada ya hapo wataruhusu kupita watu wenye dharula kama wagonjwa .
Daraja la Tulila linaunganisha Kijiji cha Mipeta na Halmshauri ya Wilaya ya Mbinga ambako wananchi wa kijiji cha mipeta na maeneo mengine wanategemea sana huduma za matibabu katika kituo cha Afya Kalembo ambacho kipo katika H/mashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Daraja la mto tulila ni sehemu iliyojengwa bwawa la kufua umeme ambao unatumika kutoa huduma ya nishati ya umeme katika Halmashauri zote katika Mkoa wa Ruvuma isipokuwa Tunduru
Aidha mfadhiri aliyefadhiri ujenzi wa bwawa na daraja hilo Bw Robat Rocker amejitolea kusaidia ujenzi wa daraja katika kijiji cha Mipeta mto Ruvuma kwa serikali kufanya upembuzi yakinifu wa awali na kuainisha gharama na yeyeyupo tayari kusaidia.
JACQUELEN CLAVERY-TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa