WATANZANIA wametahadharishwa kuchukua tahadhari dhidi ya matumizi ya bidhaa za plastiki ambazo zinatajwa kuleta athari za kiafya na kimazingira ahadhari hiyo imetolewa na Mratibu wa Baraza la Taifa la Mazingira(NEMC) Kanda ya kusini Bw Lewis Nzali katika mkutano wa taarifa ya uharibifu wa mazingira uliofanyika hivi karibuni mjini songea.
Bw Nzali amesema Watanzania wachukue tahadhari dhidi ya matuzimizi ya vifaa vilivyotengenezwa kwakutumia plastiki kwasababu vinamadhara makubwa kwa afya ya binadamu na wanyama kwakuwa vinatengenezwa kwa kutumia gesi asilia au petroliamu ambazo zinaviambata vyenye sumu na kuathiri afya ya binadamu.
“Matumizi ya vifaa hivyo vinasababisha madhara kupitia kwenye maji,udongo na hewa ambapo binadamu na wanyama wanaishi na kupata mahitaji mbalimbali muhimu kwa matumizi ya kila siku’’,amesema.
Ameyataja baadhi ya madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa hivyo ni mabadiliko ya kimaumbo kwa wanaume na wanawake kama vile wanaume kuwa na maziwa makubwa kuliko kawaida,kukosa nguvu za kiume,kuzaa watoto wasiokuwa wa kawaida,kansa,magonjwa ya njia ya hewa,mimba kuharibika kuvimba mwili,na hatimaye kusababisha vifo katika jamii.
Bw Nzali amesema uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya vifaa vya plastiki ni kifo kwa binadamu na viumbe hai wengine kwakusababisha uharibifu wa hali ya hewa wakati wa kuchoma taka, kuwaashia moto majumbani badala ya mafuta ya taa,mifuko kwa ajili ya kubebea vyakula kama chipsi vyakula mbalimbali na matumizi mengine.
Matumizi mengine ni vifungashio kwenye bidhaa mbalimbali,barafu karanga, chupa za plastiki za soda,kapeti na midoli ya kuchezea watoto
Watanzania wachukue tahadhari dhidi ya matumizi ya vifaa nya plastiki ambavyo vimebainika kuwana madhara ya kiafya kwa binadamu na viumbe hai wengine .
Sera ya mazingira ya mwaka 1997 inaelekeza pawepo na mazingira salama kwa ajili ya uzalishaji wa mazao,upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote ya mijini na vijiji na hali ya hewa safi na salama.
Imeandaliwa na Jacquelen clavery
Kaimu,Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Novemba 7,2018
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa