Watakao kwepa kutoa ushahidi kukikiona
Wananchi watakao kwepa kutoa ushahidi wa kesi mahakamani kikiona
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa TAASISI YA KUZUI NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU) Mkoani Ruvuma Yustina Chagaka wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kuanzia julai 2017 hadi juni 2018 kwa vyombo vya habari katika ukumbi wa Taasisi hiyo hivi karibuni.
Chagaka amesema kesi nyingi zinazo husu maswala ya rushwa zimekuwa zikifutwa kwa sababu ya kukosa ushahidi wa kutosheleza toka kwa wananchi wanaotakiwa kutoa ushahidi kwa kushindwa kufika au kutoa ushahidi wa uongo mahakamani.
kufuatia hali hiyo wananchi watakao shindwa au kukwepa kutoa ushahidi wa kesi za rushwa mahakamani watasakwa na kuchakuliwa hatua za kisheria .
Ameongeza kwa kusema kwa kipindi cha julai 2018 hadi juni 2018 Taasisi imefanikiwa kuokoa Zaidi ya shilingi milioni 53 katika sekta za Afya,Elimu na Tamisemi ambazo ni mishahara hewa kwa watumishi.
Aidha TAKUKURU Mkoani Ruvuma imejipanga kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo kuona kama zinatumika kwa malengo yaliyo kusudiwa,kufanya utafiti katika idara zinazo lalamikiwa ili kubaini mianya ya rushwa na kuendelea kutoa Elimu kuhusu madhara ya rushwa katika jamii.
TEHAMA- JACQUELEN CLAVERY
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa