Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Mhe Menasi Komba ameonya watakao kiuka maadili ya kazi yao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali.
Mhe.Komba ametoa onyo hilo katika kikao cha kuwaapisha madiwa kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Mji mdogo wa Peramiho hivi karibuni.
Komba amewaonya madiwani na watendaji wa Halmashauri kuzingatia maadili,miko na mipaka ya kazi zao ili kuepusha migongano katika kutekelaza majuku waliyo kasmiwa na serikali.
“Nataka Halmashauri yangu iongoze kwa mapato ya ndani ya Mkoa kwani kuna fursa nyingi bado hazijafanyiwa kazi” amesema Mhe Komba.
Komba ametaka kila idara na kitengo kukusanya mapato kupitia chanzo chake cha mapato pamoja na kuibua vyanzo vipya vya mapato, na kuangalia tozo na ushuru ambao ni kero kwa lengo la kuwasaidia wananchi
.Ameongeza kwakusema wananchi wasianzishe miradi ya ujenzi wa maboma pasipo kibali cha Halmashauri kwasababu yapo nje ya utaratibu wa bajeti ,yaliyojengwa yafanyiwe kazi ili yaweze kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.
Kwaupande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro ametoa rai kwa madiwani kujiepusha na maslahi binafsi na kujua mipaka ya kazi yao katika kuwatumikia wananchi wao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Simon Bulenganija amewahahidi madiwani kufanya kazi kwa uaminifu na ushirikiano kwakuweka mipango na utaratibu wa pamoja katika kutatua changamoto za Halmashauri.
Jumla ya madiwani 22 wameapishwa kati yao wa Kata wakiwa 16 na wa viti maalumu sita.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari Songea DC
14,12,2020.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa