TIMU ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakiongozwa na Afisa Mipango Bw. Nyange Athuman wamefanya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa Songea Vijijini.
Ufuatiliaji huo umefanyika katika shule ya msingi maleta ambapo kuna ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili viliyoanza kujengwa na nguvu za wananchi na Halmashauri imepeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 16 kwaajili ya ukamilishaji.
Pia wamefanya ufuatiliaji katika shule ya msingi Muungano ambapo kuna ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili, pia vyumba hivyo vilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi na Halmashauri imepeleka fedha kiasi cha milioni 25 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Vilevile wametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa hospitali ya Wilaya Mpitimbi ambayo inajengwa kupitia fedha za mradi wa TASAF, mradi huo ulitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 68,376,000 kwaajili ya ujenzi wa nyumba hiyo. Pia wametembelea na ujenzi wa kichomea taka kinachojengwa katika hospitali hiyo.
Mwisho wamefanya ufuatiliaji wa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa shule ya sekondari Litapwasi ambayo inajengwa mbili kwa moja na imegharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 50 hadi kukamilika.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa