Serikali kupitia OR-TAMISEMI Imewakabidhi Waratibu Elimu Kata pikipiki kwa lengo la kufutilia utendaji kazi na kuhakikisha kiwango cha taaluma kinapanda katika Halmashauri ya wilaya ya songea
Kauli hiyo imetolewa mkuu wa wilaya ya songea Mh Pololet Mgema katika hafla fupi ya kuwakabidhi waratibu elimu kata pikipiki 16 wa kata zote ilyofanyika katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya songea hivi karibuni.
Mh Mgema amewataka waratibu Elimu kata kutumia pikipiki walizopewa kwa malengo yaliyo kusudiwa pamoja na kufutilia utendaji kazi wa Elimu na kuhakikisha kiwango cha taaluma kinaongeza zaidi
Mh Mgema amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh Dkt John Pombe Magufuli imejidhatiti katika kuhakikisha inaendelea na uboreshaji wa utoaji wa huduma za jamii zikiwemo Elimu,afya Ujenzi wa miundo mbinu ya maji na barabara na utoji wa vitendea kazi kwa wafanyakazi nia ikiwa kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Adha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh Rajabu Hassani Mtiula amesema kulingana na jiofrafia ya Halmamashauri yake usafiri kwa waratibu Elimu kata ilikuwa ni changamoto katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo,hivyo upatikanaji wa usafiri wa pikipika utawasaidia kutekeleza majukumu yao kwa wakati na amewataka kutunza pikipiki hizo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Simoni Bulenganija amesema serikali imewarahisishia kazi hivyo wafanye kazi na kuleta mabadiliko makubwa ya kitaaluma katika Elimu ya Msingi,Sekondari na katika Stadi za kusoma,kuhesubu na kuandika ( KKK) na kuacha kisingizio cha kukosa asafiri pale wanapotakiwa kwenda kufanya shughuli za ufutiliaji Elimu.
Prospa Njiwa ni moja kati ya waratibu walionufaika na pikipiki hizo akizungumza kwa niaba ya wengine ameishukuru serikali kwa kuwapatia usafiri ambao utawasaida kutatua changamaoto kwa kwa upande wa usafiri kuwafikia watendajiwa wanao wasimamia na umewarahishia sana kazi
JACQUELEN CLAVERY-TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa