WANASIASA wameonywa kutoingilia kazi zinazofanywa na watalaam
Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma mh Oddo Mwisho wakati wa kikao cha viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya na wataalam wa Halmashauri ya Madaba na Songea vijiji kilicho fanyika katika ukumbi wa CCM Manispaa ya songea hivi karibuni.
Mhe Mwisho amesema wanasiasa wasiingilie kazi za wataalam kwasababu kazi hizo ni za kitaalam na wao wawe wasimamizi kwa mujibu wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapiduzi invyowaelekeza kukagua miradi ya maendeleo kila baada ya miezi mitatu.
Amesema mwingiliano wa utendaji kazi baina ya wanasiasa na wataalam unasababisha usimamizi mbovu wa miradi na mingine kutekelezwa chini ya kiwngo jambo ambalo halileti tija kwa serikali na wananchi kutopata huduma stahiki kwa wakati.
Maelekezo yanayotolewa na wanasiasa katika utekelezaji wa miradi yamekuwa ni vikwazo vya kukwamisha utekelezaji wa miradi na utoaji wa huduma kwa wananchi,wanasiasa wawe wasimamizi na kushauri nasiyo kutao maelekezo ya kiutalaam.
“ Usijivunie taaluma yako bali jivunie matokeo chanya ya kazi ya taaluma yako,”alisema Mwisho na kuongeza kuwa Serikali inatoa pesa nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo hivyo wataalam waachwe watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria,sera na taratibu zilizopo..
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Nelly Duwe amewataka wanasiasa na wataalam kuendelea kuchapa kazi kwakila mtu katika eneo lake nakuacha visingizie visivyokuwa na maana katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya serikali.
Mifumo ya mabadiliko ya uongozi katika serikali ya awamu ya tano inayoongozw na Dkt John Pombe Magufuli inalengo la kujenga na kukuza mahusiano baina ya viongozi wa chama na serikali katika kuijenga Tanzania kuelekeauchumi wa kati.
Jacquelen clavery -tehama
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa