Msimamizi wa asilimia kumi(10) ambazo ni nguvu za wananchi katika mradi wa ujenzi wa stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea Evagrini Kongwa amewaomba wananchi kutoa ushirikiano hasa katika utunzaji wa vifaa vya ujenzi ili kukamilisha ujenzi huo kwa viwango sahihi.
Ameyasema hayo ikiwa utekelezwaji wa mradi huo umekwishaanza kwa kusafisha eneo ambapo pia kupitia nguvu za wananchi wamesogeza maji katika eneo la mradi ili ujenzi huo uanze maramoja. Amesema
“Shughuli ambazo tumefanya kwanza kabisa tumesafisha eneo ikiwa ni pamoja na kung’oa miti na kuweka eneo katika hali ya usawa (leveling) kwaajili ya kuanza shughuli nyingine kama vile kuchimba msingi na hatua nyingine za ujenzi, pia shughuli nyingine ambayo tumefikia mpaka sasahivi tayari tumeshaingiza maji katika eneo la mradi kama mchango wa nguvu za wananchi, baada ya hapo tunampango wa kujenga ghala (store) la muda kwaajili ya kuhifadhia vifaa, pia tutajenga choo cha muda kwaajili ya matumizi ya mafundi na wanafanyakazi wengine katika mradi huu, pia tunampango wa kuchimba mabwawa (malambo) kwaajili ya kuhifadhia maji ili kuwarahisishia mafundi watakapoanza ujenzi basi wasipate changamoto ya maji”.
“Kimsingi naomba nitoe rai kwa wananchi ambao wanauzunguka mradi huu kuweza kutunza mali au vitu tutakavyokuwa tunavileta hapa kwaajili ya shughiuli za ujenzi maana hizo ni mali zao kwani mali za Serikali ni mali za wananchi kwahiyo niombe kila mwananchi kuwa mlinzi kwa mwenzake katika kulinda mali hizo, pia natoa wito kwa wafanyakazi wa Halmashauri kuweza kutoa ushirikiano hata kwa ushauri tu kama kuna sehemu haijakaa sawa ni vema wakatoa ushauri ili kuboresha mradi huu na Halmashauri yetu ikapendeza kwa kupata stendi nzuri na yakisasa”
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Songea Ndug Neema M Maghembe, ameendelea kusisitiza kwa viongozi wote wanaohusika na kusimamia mradi huyo, kuhakikisha shughuli zinaenda kwa kufuata utaratibu na kujali muda waliopewa kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Stendi hiyo.
“ Niendelee kuwasihi wasimamizi wa mradi huu, kusimamia vema ujenzi wa hii stendi, kwani uwepo wa stendi hii unafaida kubwa kwa wananchi wa Lundusi na Halmashauri kwa ujumla. Hivyo naamini watendaji wetu watajali muda tuliopewa wa kukamilisha ujenzi huo na kusimamia kwa weredi shughuli zote za ujenzi zinazoendelea. Tutaendelea kutoa ushirikiano kwa wataalam wetu wote kuhakikisha hawakwamishwi na chochote katika kutekeleza majukumu yao.
Mradi huu wa ujenzi wa stendi ulizinduliwa rasmi tarehe 16/08/2023 na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe.Jenista Joakim Mhagama na utaghalimu kiasi cha shilingi 434,657,802.68 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu kupitia TASAF na unatarajiwa kukamilika mwaka 2025
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa