Wananchi wa Halimashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wameshauriwa kujenga vyoo bora na kuboresha usafi wa mazingira.
Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Usafi na Mazingira wa Halmashauri hiyo John Kapitingana wakati akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi bora ya vyoo ofisini kwake.
Kapitingana ameeleza sifa ya choo bora ni kuwa na sakafu safi inayo safishika vizuri,kuta imara zinazotunza faragha, paa rafiki,hakiruhusu mazalia ya wadudu ,sifa nyingine ni kuwa na maji tiririka maeneo ya chooni na sabuni ya kunawa baada ya kujisaidia.
Amesema wa vyoo bora na uboreshaji wa mazingira utasaidia kupunguza magonjwa ya matumbo kwenye jamii.
Amezitaka kamati za kampeni za usafi wa mazingira zilizoundwa kila kijiji kuhakikisha zinaendelea kuhamasisha wananchi kujenga vyoo bora na kuvitumia kwa usahihi katika makazi yao.
Ametaja magonjwa yanayotishia uhai wa binadamu yanayo sababisha na utupaji wa kinyesi hovyo kuwa ni minyoo,kichocho tumbo,homa ya matumbo kama vile kuhara damu na kawaida ambayo yanaweza kuepukika kwa kuzingatia kanuni za afya na matumizi bora ya vyoo.
“ujenzi wa nyumba bora na za kisasa uende sambamba na ujenzi wa vyoo bora”,alisema Kapitingana.
Aidha amesema upimaji wa zoezi mashindano dhidi ya kampeni ya usafi wa mazingira ambalo limeshaanza tangu tarehe 1/05/2019, Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni miongoni mwa wilaya zilizochaguliwa katika kampeni hiyo na vigezo ni usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya.
Jacquelen Clavery-k /Afisa Habari .
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa