Wanachi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wameungana na Watanzania wenzao katika kuomboleza kifo cha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kilicho tokea machi 17,2021 Jijini Dar es salam.
Wananchi wa kijiji cha Peramiho ( b) wamesema wamesikitishwa sana na kifo cha Dkt. Magufuli kwasababu aliwaweka watanzani wote katika kapu moja bila kujali tofauti za kidini na itikadi za kisiasa.
Wamesema wanatoa pole kwa Chama cha Mapinduzi na Serikali kwa msiba huu na kumwombea kwa Mungu amlaze mahala pema peponi katika hii dunia hakuna atakayebaki kwakuwa kifo kimeumbwa.
Andrea Nzali na Adam Ngunga ni miongoni mwa waombolezaji wamesema wamepokea kwa masikitiko na uchungu mkubwa kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Watanzania kwakuwa ni kiongozi shupavu na aliyesimamia kwa vitendo dhana ya uwajibikaji pasipo kumwonea mtu yeyote.
Wameongeza kwakusema Rais Magufuli ni kiongozi wa kuigwa Barani Afrika kwasababu alionyesha kwa vitendo katika kusimamia rasilimali za nchi.
“BWANA ALITOA,BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa