SERIKALI imetoa Shilingi Milioni 400 kwaajili ya kutekeleza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Magagura.
Akizungumza Mganga Mkuu wa Wilaya Geofrey Kihaule amesema kituo hiki kinahudumia wananchi wa Kata ya Magagura, Kizuka, Mbinga Mhalule pamoja na vijiji vyake.
‘’ Kituo kina majengo manne jengo la wagonjwa wa nje, jengo la maabara, majengo mawili yameungana ambayo ni jengo la mama na mtoto na jengo la upasuaji’’, amesema Dkt Kihaule.
Dkt Kihaule amesema kituo kilianza kutoa huduma mwezi Desemba 2021 kwa huduma za wagonjwa wa nje.
Kwaupande wake Daktari wa Kituo cha afya cha Magagura Rebecca Kanju ameeleza kuwa kituo cha Afya kinahudumia wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo ni Malaria, macho, meno, presha ya kupanda, maambukizi ya njia ya mkojo, vidonda vya tumbo na magonjwa ya mfumo wa upumuaji.
Wakizungumza wananchi wa Magagura wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho kwa kuwaletea fedha za kujenga kituo cha Afya.
Pia wamewashukuru Baraza la Madiwani linaloongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhe.Menas Komba, Mkuu wa Wilaya Mhe.Pololet Mgema, Viongozi wa Chama pamoja na timu ya Wataalamu wanaoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Neema Maghembe kwa kutekeleza na kusimamia mradi huu wa kituo cha Afya.
Wamesema kabla ya ujenzi wa Kituo hiki walikua wanalazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma katika zahanati ya Chipole hivyo kituo kimesaidia na kimewarahisihia kupata huduma kwa haraka.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa