Wananchi wa Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma wamepongeza na kutambua jitihada za Mbunge wao Mh Jinista Mhagama katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo.
Wamesema kwa nyakati tofauti katika maadhimisho ya wiki ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) yaliyo fanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Namatuhi Wilayni songea.
Wananchi wamesema wanatambua umahiri na jitihada zinaofanywa na Mbunge katika kuchangia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za kijamii katika makazi yao.
“Chifu wa wangoni Emanueli Gama anamfananisha Mh. Mhagama na Mtawala wa 7 wa Misri Malkia CLEOPATRA sio kwa uzuri bali kwa uhodari wake wakuchapa kazi bila kuchoka ndo maana Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alimteua kuwa waziri”alisema chifu Gama.
Graceana Ntanga ni miongoni mwa wananchi wa jimbo la Peramiho anasema anatambua umahiri wa Mh. Mhagama katika swala zima la kuwasaidia wananchi kwa vitendo na michango ya fedha katika uanzishaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Mh. Mhagama amekuwa kiongozi mahiri na mfano wa kuigwa katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo kwa wananchi kwakutoa michango ya mawazo, ushauri na fedha katika miradi ya maji hususani uchimbaji wa visima ambavyo vimechimbwa takribani maeneo yote ya Jimbo la Peramiho, ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, umeme wa jua, ujenzi wa miundo mbinu ya mashule, Zahanati, SACCOS, vikundi mbalimbali vya wanawake na Vijana na vifaa mbalimbali vya viwandani
Aidha Mh. Mhagama amewasaidia wananchi kwa kuanzisha shule shikizi za Ulamboni,Lunyele Maleta,Jenista,Mborongo, nyingine ni Lihuhu, Ligunga, Mhimbasi na Selekano ambazo wananchi walikuwa wakimwomba kuanzishiwa shule hizo kwasababu ya wao kuhama toka makazi yao ya awali na kutafuta maeneo kwa ajili ya shughuli za kiliomo hivyo kushindwa kumudu umbali mrefu wa kuwapeleka watoto wa kupata Elimu kwenye shule mama.
Imeandaliwa na jaccquelen Clavery kaimu Afisa Habari Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa