“WANANCHI hangaikeni na Shughuli za Maendeleo” ambazo zitawasaida kuinua uchumi kuelekea kwenye uchumi wa kati wa viwanda
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye ulemavu Mh. Jenista Mhagama kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika Kata za Litisha, Maposeni, Magagura na kata ya Kilagano wiayani Songea hivi karibuni.
Mh.Mhagama amesema wananchi wahangaike na shughuli za maendeleo ambazo zitawaletea maendeleo ya kiuchumi kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa na kujitolea katika kazi mbalimbali kama vile Ujenzi wa Maboma ya Zahanati, Shule, ufyatuaji wa tofari na Miundombinu.
Mh.Mhagama amewahaidi wananchi wa kata alizozitembelea kuwatatulia kero mbalimbali kama vile maji kwa kuwachimbia visima vyenye ureufu wa mita miamoja na hamsini ambavyo vitasaidia kutatua tatizo la maji kwa wananchi.
Kero nyingine ni umeme, Miundombinu ya barabara na vifaa vya viwandani ambavyo vitasaidia kukamilisha ujenzi wa Zahanati katika vijiji ambavyo vimejenga maboma ya Zahanati.
Aidha amewapongeza wananchi wa kijiji cha Lusonga kata ya Magagura tawi la Muungano kwa maamuzi ya kufyatua tofari Laki moja na ishirini kwaajiri ya kuanzisha mkondo wa shule ambapo wanatarajia kujenga vyumba vitatu vya madarasa, Nyumba moja ya mwalimu na Choo na kuwataka wananchi wengine kuiga mfano huo.
Katika kuunga mkono jitihada za wananchi wa Lusonga tawi la Muungano Mbunge huyo wa Jimbo la Peramihi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye ulemavu Mh. Jenista Mhagama amewachangia kiasi cha shilingi Laki tano (500,000/=) kwa ajili ya kuchoma tofari hizo.
JACQUELEN CLAVERY-TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa