Ujenzi wa zahanati ya Lipaya kata ya Mpitimbi wilayani Songea mkoani Ruvuma utasaidia kupunguza tatizo la kujifungulia njia kwa akina mama wajawazito na vifo kwa watoto wachanga.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wakazi wa kijij hicho kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na kamati ya fedha, utawala na mipango.
Wamesema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia kupunguza tatizo la akinamama wajawazito kujifungulia njiani wanapoenda kujifungua katika hospitali ya peramiho au hospitali ya mkoa zaidi ya umbali wa kilomita 10 na wakati mwingine hufia njiani au kupata matatizo ya kiafya.
“Wanasema tunapata shida kwa upande wa huduma za matibabu kwa kuwa wanalazimika kutembea umbali wa kilomita nane kuelekea Mpitimbi kwenye zahanati na mwendo wa zaidi ya kilomita 10 kufuata matibabu katika hospitali ya Mkoa au Peramiho’’, Alisema Veronika Komba na Danieli njovu.
Ujenzi wa zahanati ulichagizwa na wananchi wenyewe baada ya kukabiliwa na changamoto za huduma za afya mwaka 1992 kwa wananchi kufyatua tofari na kujenga boma kupitia michango yao na mbunge kuwachangia kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni mbili na serikali 2018 imetoa shilingi milioni 97,500,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi na kujenga nyumba moja ya mtumishi ,ujenzi ambao umefikia asilimia 75
Zahanati ya Lipaya ni miongoni mwa zahanati nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambazo zinatarajiwa kupandishwa hadhi kuwa vituo vya Afya.Zahanati nyingine ni Nakahegwa,Mpingi na Lugagara.
Mbunge wa Jimbo hilo Ndg Jenista Mhagama aliomba kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Kassimu Majaliwa Kassimu baada ya kufanya ziara katika Halmashauari ya Wilaya ya Songea Januari mwaka huu.
JACQUELEN CLAVERY . TEHAMA- HABARI 31.01.2019
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa