Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wameshauriwa kuwa na shamba la pamoja la mazao ya kimkakati kwajili ya kunufaika na fursa za kilimo na kuongeza kipato.
Ushauri huo umetolewa na Afisa kilimo wa Halmashauri hiyo Hellne Shemzigwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Magwamila kilichopo Kata ya Mhukuru Lilahi.
Shemzigwa amefafanua shamba la pamoja kuwa ni shamba linalotekelezwa na wananchi,Taasisi,Mashirika na Makampuni kwa kulima eneo moja lililotengwa na kukubaliwa na Serikali ya Vijiji kwa lengo la kulima mazao ya kimkakati ambayo ni alizeti,ufuta,soya na korosho na mazao mengine ambayo yanatoa fursa kwa wakulima.
Katika kufanikasha adhima hiyo Halmashauri imeanza uhamasishaji kwakufikia wananchi na kuwapa elimu kuhusu umuhimu wa kilimo cha pamoja kwa njia ya mikutano ya hadhara na wananchi wamekubaliana na mpango huo.
Shemzigwa amezitaja faida za kuwa na shamba la pamoja kuwa ni kuzalisha ajira ndogondogo,uratibu wa masoko ambao unafanywa na Serikali,kuongeza uzalishaji,urahisi wa usimamizi na ufuatiliaji na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la Serikali.
Shemzigwa ameongeza kwa kusema kwa Upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mazao ambayo yanapendekenzwa kwakuanzia ni korosho zao ambalo linastawi katika maeneo yawastani,na zao la alizeti zao ambalo linastawi katika maeneo yote ya Wilaya hiyo.
Kwa upande wao wananchi wa Kijiji cha Magwamila wametenga eneo lenye ukubwa wa hekari 500 kwa ajili ya kilimo cha zao la korosho zao ambalo linastawi vizuri sana katika Kata hiyo na Kata ya Muhukuru Barabarani.
Uzalishaji wa zao la korosho katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea umeshuka hadi kufikia chini ya tatu kufutia serikali kusitisha zoezi la ugawaji wa ruzuku jambo lililopelekea wakulima kutelekeza mashamba yao na kuhamia kwenye kilimo cha mazao mengine.
Kilimo chapamoja ni kilimo kikubwa ambacho kinaenda sawa na kilimo cha mkataba kilimo ambacho mkulima anaingia mkataba na makampuni kwa kupewa pembejeo za kilimo kwa makubaliano baada ya mavuno mkulima atawajibika kuuza mazao yake kwenye kampuni husika.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
SongeaDC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa