Mkuu wa wilaya songea mkoani Ruvuma pololet Mgema ameagiza wahudumu wa afya ngazi ya jamii wajengewe uwezo dhidi ya mapambano ya utekelezaji wa afua za lishe.
Mgema ametoa maagizo katika kikao cha Lishe cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mgema ametoa agizo hilo kufuatia tatizo na madhara ya Lishe duni kuendelea kuwepo katika jamii wakati fursa na mahitaji ya msingi ya kupambana na tatizi hilo yapo na yanaptikana katika ngazi ya jamii.
“Ukiukaji wa miongozo,taratibu na sheria za Lishe unasababisha afua za lishe kutotekelezwa vizuri”,ameonya Mgema.
Ametaka sheria,taratibu na miongozo ya utekelezaji wa afua za lishe uzingatiwe kwa malengo yaliyopangwa ya kukabiliana na tatizo la lishe duni kuanzia ngazi ya jamii hadi Kimataifa.
Kwa upande wake Afisa lishe wa Wilaya hiyo Joyce Kamanga ameyataja madhara yatokana nayo na lishe duni kuwa ni maradhi ya mara kwa mara,uwezo mdogo wa kufikiri,kudumaa kiakili,kupoteza kumbukumbu na wakati mwingi kusababisha vifo.
Halmashauri ya wilaya ya songea inajumla ya wahudumu wa afya ya ngazi ya jamii 112 ambao wanafanya kazi katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa