Wafugaji wa Elimishwa kuhusu umuhimu wa kufuga kwa njia ya vitalu.
Wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wameelimishwa kuhusu umuhimu wa kufuga kwanjia ya vitalu ,ufugaji a mbao utaleta tija kwa wafugaji naTaifa pia utapunguza kwakiasi kikubwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji .
Elimu hiyo imetoleawa na Daktari wa mifugo wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Ramadhan I Mwaiganju katika mkutano wa wafugaji wakubwa na wadogo na wataalamu wa mifugo wa Mkoa na Wilaya uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Dkt Mwaiganju amesema ufugaji kwa njia ya kitalu unafaida kubwa kwa jamii na wafugaji wenyewe kwasababu utasaidia kuondoa migogoro baina yao na wakulima,wafugaji kumiliki ardhi badala ya kuhamahama,pia utasaidiakuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kudumisha hali ya lishe katika kaya kutokana na mazao ya tokanayo na mifugo hiyo.
Ameitaja mikakati ya baadaye ya kuwawezesha wafugaji kuishi katika mazingira bora zaidi ni kuwajengea uwezo wa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa mahoteli,nyumba za kulala wageni, maduka ya vinywaji ,maduka ya nyama na viwanda vidogovidogo.
Awali akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashaurihiyo Bw Simoni Bulinganija amewataka wagufaji kuzingatia mabadiliko ya kisera yenye lengo la kuboresha na kuleta tija katika sekta ya mifugo kuelekea uchumi wa kati waviwanda.
“Nchi inaingia katika uchumi wa kati waviwanda wafugaji mnachango mkubwa hivyo muone namna gani mtasaidia,”alisemaBulengaji.
Kwa upande wao wafugaji wamefurahishwa na utaraibu ambao serikali inawata kufuga kupitia vitalu, nao wapo tayari kuutekeleza. Kwasababu utawanufaisha kwakuachana na tabia ya chuki ambayo waliiona kama njia moja wapo ya kupambana na wakulima pindi mifugo yao inapoharibu mazao ya mkulima na kutambuliwa kisheria tofauti na ufugaji awli.
Mkoawa Ruvuma unawafugaji 321 wakubwa na wafugaji wadogo 17 wakati Halmashauri ya Wilaya ya Songea inawafugaji 91 wakubwa na wadogo ni zaidi ya 800,aidhaHalmashauri imetenga vitalu 160 katika vijiji vya Mhepai ,Magwamila na Nambendo.
NA JACQUELEN CLAVERY-SONGEA DC
KAIMU AFISA HABARI.
28 / 08/ 2019.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa