Wafugaji wa kuku wa Kijiji cha Nakahegwa ,Kata ya Mbinga Mhalule wameshauriwa kutumia teknolojia rahisi katika kufanikisha malengo yao ya ufugaji ili waweze kupata mafanikio ambayo yatawawezesha kupunguza umasikini wa kipato katika kaya zao.
Ushauri huo umetolewa na Afisa mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Dr Erick Kahise katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wafugaji kuku wa kikundi cha federation moja kilichopo katika kijiji cha Nakahegwa.
“Ufugaji utawasogeza mbele,”amesema Dr Kahise
Dr Kahise amesema ili mfugaji aweze kupata mafanikio chanya afuate kanuni na taratibu za ufugaji kupitia teknolojia rahisi ikiewemo ujenzi wa mabanda ya kawaida ambayo vifaa vyake vinapatikana katika mazingira yao wanayoishi mfano miti na nyasi.
Ameongeza kwa kusema wafugaji wafuge kitaalam kwa kuwashirikisha wataalam wa mifugo kuanzia hatua ya awali ya utayarishaji wa banda, matumizi ya chanjo na utengezaji wa chakula ambao unafaa kulisha kuku.
Dr Kahise amesema ufugaji usiozingztia kanuni na taratibu za ufugaji unasababisha hasara kwa wafugaji kufuatia kuku hasa vifaranga kukumbwa na magonjwa na vifo jambo linalo rudisha nyuma jitihada za kujinasua na umaskini wa mtu mmoja mmoja au kaya.
Kwa upande wake mlezi wa kikundi hicho Remigiusi Mbawala amesema kikundi hicho ni cha hiari ambacho kina mtaka kila mwanachama kutekeleza majukumu yake bila shuruti na aweze kujipatia kipato chake kupitia mradi wa ufugaji kuku.
Naye mratibu wa kikundi hicho Sponsa Dimayo amewaomba wataalam wa mifugo kuwatembelea na kuwapa elimu na ushauri ambao utawasadia kubadili mitizamo ya kufuga kwa mazoea na kufuga kisasa.
Naye Mratibu wa mfuko wa wanawake kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii Xveria Mlimira amewataka wanakikundi kutimiaza vigezo vya kukopeshwa ili waweze kukopeshwa mikopo inayo tolewa na Halmashauri na vigezo ni kufungua akaunti na kuhakikisha kazi yao ya ufugaji inakuwa endelevu.
Kikundi cha Fideration Moja kinajumla ya wanachama 12 ambao wanajishugurisha na shughuri ya ufugaji kuku na kilimo cha mazao ya bustani na kimeanzishwa mwaka 2016.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa