Viongozi wa dini wamedai uyumbishwaji wa taarifa za awali kuhusu chanjo ya UVIKO-19 zilizokuwa zikitolewa na wataalam wa Afya zilikuwa na mkanganyiko ndani yake jambo lililosababisha baadhi yao kukinzana na Serikali katika juhudi za pamoja katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.
Madai hayo wameyasema katika kikao cha tathimini ya Afya ya Msingi cha Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea hivi karibuni katika
“Awali maelekezo mliyokuwa mkiyatoa wataalam wa Afya yalikuwa yanatuchanga na tulishindwa kuelewa,lakini kwa sasa tumeelewa na tunawaelimisha wa umini wetu juu ya umuhimu wa kuchanja chacho ya UVIKO -19 na maswali yamepungua,” Padre Fredrick Mwabena amesema.
Mwabena amesema maelekezo yaliyokuwa yanatolewa awali na wataalam sekta hiyo yalikuwa na mkanganyiko jambo ambalo na wao kama viongozi wa dini walibaki njia panda ya kusaidi kuelisha waumini wao umuhimu wa kuchanja chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa korona.
Shekhe Saidi Rashidi Namawela naye anakili kuhusu kuwepo kwa taarifa za uyumbishaji kuhusu chanjo ya UVIKO-19 jambo ambalo liliwapa shida katika kuamini upi ni ukweli na upi ni uongo ,lakini kadri elimu hiyo inavyo endelea kutolewa wao wameelimika na kuunga mkono jitihada za Serikali za mapambao ya dhidi ya ugonjwa wa korona.
Akizungumzia kuhusu chanjo mpya aina ya sinopharm Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Geofrey Kihaule amesema Halmashauri ilipokea mgao wa chanjo 3572 ambazo mtu aliyehiari kuchanja atachanja awamu mbili,na tayari zoezi limefanyika na limekamilika.
Kihaule amesma wale wote waliochanja awamu ya kwanza,awamu ya pili watachanja chanjo nyingi baada ya siku 21 hadi 28 kwa utaratibu wa majina yao kubandikwa kwenye mbao za matangazo karibu na makazi yao na tarehe ambayo watatakiwa kuja kupata chanjo awamu ya pili.
Naye mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amewapongeza wataalam wa Afya kwa zoezi la uchanjaji ambalo kwa Halmashauri ya wilaya ya songea linaendelea vizuri,pia ameshauri uhamasishaji uendele na wananchi wa Vijiji vyote wafikiwe ili wanaohiari kuchanja wapate huduma hiyo.
Amewasisitiza wataalam wa Afya kujifunza kutokana na changamoto wanazokutanazo katika utekelezaji wa zoezi la utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 ambazo zitawasaidia kujenga uelewa zaidi wa kukabiliana na tatizo hilo ambalo bado linaendelea kuteketeza maisha ya watu.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa