Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya Matawi kutumia rasilimali zilizopo kuimarisha uchumi wa chama hicho
Mwisho ametoa maagizo hayo katika maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa ccm yaliyofanyika februali 5,2021 katika uwanja wa michezo wa Wilaya Mbinga.
Mwisho amesema viongozi wawajibike kutumia rasilimali mbali mbali za chama kama ardhi,kuendeleza majengo ya zamani na vyanzo vingine vya mapato kwa lengo la kukiimarisha chama kiuchumi ili kiweze kujitegemea na kujisimamia chenyewe.
Mwisho ametoa mwito kwa viongozi wa ccm wa ngazi zote kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu wanapowatembelea kutoa kero zao kwa lengo la kusaidiwa.
“Endeleeni kukitumikia chama chenu”amesema Mwisho.
Amewapongeza wanachama wa ccm waliomba nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2020 na hawakubahatika kupata nafasi na bado wanaendelea kutoa ushirikiano kwenye chama waendelee kukitumikia chama chao katika misingi ya kuijenga nchi yetu.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na shughuli za ukaguzi wa miradi mbalimbali ya chama ambayo ni majengo ya Shule ya Sekondari pamoja na matundu ya vyoo,yaliyo jengwa katika kata ya Mateka ,jengo la Ofisi ya Serikali ya mtaa katika kata ya Matarawe,ujenzi wa vibanda 22 vya biashara katika uwanja wa michezo,kata ya Mbinga mjini pamoja na ujenzi wa Ofisi ya ccm ya Wilaya ya Mbinga.
Imeandikwa na,
Jacquelen Clavery,
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa