Vijiji sita vya Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kunufaika na mradi wa mnyororo wa kuendeleza thamani wa mazao ya misitu ambayo ni mbao, mkaa na asali
Hayo ameyasema mratibu wa mradi huo Mkoani Ruvuma bw Tengule Mutunda katika mafunzo ya kuutambulisha mradi kwa madiwani na watendaji wa Halmashauri yaliyo fanyika havi karibauni katika ukubi wa Halmashauri hiyo.
Vijiji sita ambavyo vitanufaika na mradi huo ni Litowa,Liweta,Kituro, Matuhi,Ndongosi na Muhukuru
Bw Tengule amesema mradi huo una matokeo chanya ya kiwemo kuimarisha thamani ya mazao ya misitu,kuendeleza uhifadhi wa misitu ya asili,uwepo wa mfumo madhubuti wa huduma za ugani,mawasiliano na ufutiliaji washughuli za misitu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema ametoa wito kwa wafadhili wa mradi kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika kwa kuwahamasisha na kuwaelisha kuelewa umuhimu wa miradi wanayopata na kuona miradi hiyo wanawajibu wa kuitunza na kuiendeleza na kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima katika jamii.
“Tumekuwa wa hifadhi wa asili kwa kutunza kumbukumbu na ujuzi wa asili kunaumuhimu wauendelezaji wa mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu ambayo yanatupeleka kwenye uchumi wakati wa viwanda kwa kutengeza bidhaa badala ya kuuza malighafi, na uimarishaji uchum wa kipato,”alisema Mgema.
Aidha mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya songea mhe Rajabu Mtiula ametoa rai kwa madiwani wote ambao wanahusika na mradi huo kutoa ushirikiano pale watakapo takiwa kufanya hivyo kwalengo la kutokwamisha maendeleo ya mradi katika jamii.
Mradi wa kuendeleza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu unatekelezwa katika mikoa ya Ruvuma,Dodoma,Tanga,na Lindi kwakipindi cha miaka mine na unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwakushirikiana na serikali ya Finland.
JACQUELEN CLAVERY
AFISA HABARI - SONGEA DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa