Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea, Ndg. Mtela Mwampamba aipongeza Halmashauri ya Wilaya Songea kwa kutekeleza utoaji wa mkopo ya 10% kwa vikundi vya kinamama, vijana na watu wenye ulemavu katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Jenista Joakim Mhagama uliopo maposeni sekondari leo Januari 8.
Ambapo vikundi vya wanawake vikiwa ni 45, vijana vikundi 30, na watu wenye ulemavu ni vikundi 8 ikikamilisha idadi ya vikundi 83 ambavyo vimenufaika na mkopo wa 10% ambao ni sehemu ya kiasi cha shilingi millioni 726 ambazo ni mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya Songea
Katika hotuba yake amewakumbusha wanufaika wa mkopo huo wa 10% kuwa ikatumike katika shughuli za maendeleo ili wakainuke kiuchumi, kwasababu serikali imetoa mikopo hio kwa mwananchi mmoja mmoja huku ikiwa na masharti nafuu bila ribaa ambayo hayatombana mnufaika kuliko mikopo ya Taasisi binafsi alisema “mikopo ni mtaji” hivyo kujikita kwenye shughuli za uzalishaji iwe ni lengo lenu kuu.
Aidha amevitaka vikundi hivyo kurejesha mikopo hio kwa wakati ili wengine waweze kukopa itakapo kuja awamu nyingine. Pia aliwapongeza kwa uthubutu na ari waliyonayo kwani “nyinyi ni watenda kazi ndio maana mmekopa na mnakwenda kujishughulisha na kuachana na uvivu” alisema hayo wakati wa hutuba yake.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndug. George Ponera alipata nafasi ya kutoa salamu za Serikali amesema kuwa “mikopo hii ni muendelezo wayale ambayo Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hasan ameyasema kuyatekeleza”. Hivyo aliwataka wanufaika hao wakatekeleze shuguli za maendeleo “Turejeshe mikopo ili wengine wenye sifa na watakaokidhi vigezo waweze kuja kukopa katika awamu zijazo.
Pia Kaimu Mkurugenzi Bi. Bumi Kasege nae alitoa rai yake kwa wanufaika hao wa mkopo wa 10% ambazo ni sehemu ya pato la Halmashauri alisema “fedha ambazo mmepokea zikatumike sawa sawa na shughuli ambazo mmeombea” pia aliwataka wanufaika hao kuiombea Halmashauri iendelee kukua katika mapato yake ili na wao wanaSongea waendelee kunufaika Zaidi katika mkopo huu 10%.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa