Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bwa. Exavery Luyagaza, leo Januari 13, 2026, amefungua mafunzo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma kwa watumishi wa Halmashauri hiyo, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kusini, yakilenga kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika ununuzi wa serikali.
Akizungumza wakati anafungua mafunzo hayo, Bwa. Exavery aliishukuru PPRA kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu, akieleza kuwa yamekuja katika kipindi muafaka ambapo Halmashauri inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayohitaji usimamizi makini wa michakato ya ununuzi.
“Mafunzo haya yatatuwezesha kuongeza uelewa wetu kuhusu Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma na yatajibu changamoto nyingi ambazo tumekuwa tukizipata katika utekelezaji wa majukumu yetu. Kupitia mafunzo haya, watumishi watajifunza kwa kina wajibu wao katika kuhakikisha ununuzi unafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa,” alisema Bwa. Exavery.
Aliongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea imejipanga kuyatumia maarifa yatakayopatikana ili kuboresha mifumo ya ndani ya ununuzi, kuimarisha usimamizi wa zabuni na mikataba, pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wote wanaohusika na shughuli za ununuzi.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo Bwa. Michael Ibrahim mtaalamu wa PPRA Kanda ya Kusini, alibainisha kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati endelevu wa mamlaka hiyo wa kuhakikisha taasisi zote za umma zinaelewa kikamilifu Sheria ya Ununuzi wa Umma na kuitekeleza kwa ufanisi, sambamba na kuimarisha misingi ya utawala bora katika ngazi zote za Serikali.

Mafunzo hayo yalifanyika katika mazingira ya kujifunza yaliyoruhusu majadiliano ya wazi, maswali na majibu, pamoja na uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizojikita katika tafsiri ya Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma, mabadiliko yaliyofanyika ikilinganishwa na sheria ya awali, pamoja na wajibu wa kila mdau katika kuhakikisha ununuzi unafanyika kwa kuzingatia misingi ya uwazi, ushindani wa haki na thamani halisi ya fedha.

Katika mafunzo hayo, wataalamu wa PPRA walieleza kuwa lengo kuu la mafunzo ni kujenga
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa