Ushiriki wa wanachi katika ujenzi wa kituo cha afya.
Wananchi wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya Muhukuru
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mh Rajabu Mtiula katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lilahi Muhukuru hivi karibuni.
Mh Mtiula amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya kwakujitolea nguvu zao na kuona ujenzi ni moja ya majukumu yao kwani kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaleta manufaa makubwa kwo pamoja na kupata huduma za afya kwa uhakika,kupunguza gharama za kufuata matibabu umbali mrefu pia nifursa ya maendeleo kwao.
Amesema serikali imetoa shilingi milioni miatano ambazo zitanunua vifaa tiba kutoka bohari kuu ya madawa,kutengeneza mifumo mbalimbali ya kisasa na kujenga majengo matano ambayo ni jengo la kinamama na watoto,chumba cha kuhifadhia maiti,chumba cha upasuaji na nyumba moja ya mtumishi.
Adha mwenyekiti wa kijiji cha Lilahi Mh Bashiru Karume amesema mtu yeyote atakaye thubutu kwenda na kinyume na makubaliano waliyojiwekea anamchukulia hatua za kisheria.
Ametoa shukurani kwauongozi wa serikali kwakuelekeleza fedha hizo zijenge kituo cha afya Muhukuru na sio sehemu nyingine.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa