UPIMAJI
Naibu wa Waziri OR TAMISEMI Josephat Kandege (mb) ameagaiza maeneo yote yaliyojengwa Zahanati na vituo vya Afya yapimwe na kupatiwa hati miliki
Mh Kandege ametoa agizo hilo alipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha Afya Muhukuru na zahanati katika kijijji cha Lipaya hivi karibuni.
Mh Kandege amesema maeneo yote yaliyojengwa vituo vya Afya na Zahanati yapimwe na kupatiwa hati miliki yaweze katambulika kisheria.
Aidha Mh Kandege ameuagiza uongozi wa Halmashauri kuhakikisha kiasi cha fedha shilingi milioni 400 zilizo tolewa na serikali zinakamilisha ujenzi wa Zahanati na nyumba ya mtumishi
Kufuatia hali hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mh Rajabu Hassan Mtiula amewataka wataalam wa idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya kuanza taratibu za kupima majengo hayo ambayo ni Kituo cha Afya Muhukuru,zahanati ya Lugagala, Lipaya,Mpingi na Nakahegwa.
JACQUELEN CLAVERY -TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa