Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepokea fedha kiasi Cha shilingi Milioni 198, 700,650 kutoka Serikali kuu Kwaajili ya ujenzi wa ghala na soko katika Kijiji cha Matomondo.
Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Menas komba katika mkutano wa hadhara wa kutambulisha mradi Kwa wananchi.
Aidha, katika mkutano huo ulioambatana na zoezi la utambulisho wa kamati ya ujenzi ambayo itasimamia utekelezaji wa mradi.
Akizungumza Mheshimiwa Komba amezitaka kamati za ujenzi kuwa na ushirikiano baina yao ili mradi uweze kukamilika Kwa wakati na viwango vinavyokubaliwa na Serikali.
" Napenda kuchukua nafasi hii kuwasisitiza kamati zote zinazohusika na ujenzi ikiwemo kamati ya manunuzi na mapokezi hakikisheni mnanunua vifaa vyenye ubora ili hili soko liweze kudumu na litumike Kwa vizazi na vizazi", amesisitiza Mheshimiwa Komba.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema maghembe ametoa shukrani Kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama Kwa kuleta fedha hizo Kwaajili ya ujenzi wa soko ambalo linaenda kusaidia wakulima kuuza mazao na kuinua uchumi.
Ndugu Neema amesema mradi ni wa wananchi wote hivyo Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha mradi unaisha Kwa muda uliopangwa.
"Tumekuja kufafanua ili Kila mmoja katika Kijiji awe na uelewa na huu mradi hivyo nawasisitiza Kila mtu aguswe afanye wajibu wake panapotakiwa nguvu za wananchi naomba mjitoe ili huu mradi ukamilike mapema", amesisitiza Ndugu Neema.
Pia amewahasa kamati zinazosimamia mradi pamoja na watumishi wanasimamia mradi kuwa waadilifu na wenye weledi mkubwa ili kuhakikisha mradi unajengwa kwa ubora na viwango vinavyotakiwa na kwa thamani halisi ya fedha
Vilevile amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuweka maslahi binafsi mbele na kwenda kinyume na taratibu za manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa mradi na usimamizi wa mradi kwa ujumla.
Akizungumza Diwani wa Kata ya Mbinga Mhalule Mheshimiwa Nasri Nyoni ameushukuru uongozi wa Halmashauri Kwa kuja kutambulisha mradi na kujenga uelewa Kwa wananchi hivyo ameahidi kushirikiana vyema na viongozi wa Kata na Kijiji pamoja na wananchi ili kuhakikisha mradi huu unakamilika Kwa viwango.
Nae Afisa Kilimo Wilaya Bi Hellen Shemzigwa amesema Serikali imeleta fedha hizo Kwa dhamira ya kusaidia mkulima ili asisumbuke na mazao hivyo amewataka wananchi wa Matomondo kuupenda na kuheshimu mradi huu Kwa maslahi yao.
Wakizungumza wananchi wa Kijiji cha Matomondo wamemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Kwaajili ya kuleta fedha za ujenzi wa soko ambalo linaenda kutatua changamoto katika uuzaji wa mazao.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa