Ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Jamii imetakiwa kutambua vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinaendelea kushamiri katika maeneo yetu tunayoishi.
Hayo yamebainishwa katika mafunzo ya siku tatu ya kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto katika Mamlaka za Serikali za Mitaaa yaliyo fanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Maliasili mjini Songea.
Jamii imetakiwa kutambua kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinaendelea kushamiri hivyo kila mwananchi anawajibu wakupambana katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto mahali alipo bila kujajili itikadi yake,umri hata kabila lake.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw. Martin Mtani ametaja baadhi ya aina ya ukatili ambao hufanyiwa wanawake na watoto ikiwa ni ubakaji ,ulawiti,vipigo ,ukatili wahisia , na matusi
Aidha, Bw Mtani ameyataja madhara ya ukatili ni pamoja na vifo kwakusababishwa na vigo na manyanyaso,ubakwaji,mimba za utotoni,magonjwa yakiwemo ya kuambukizwa kuathirika kisaikolojia,visasi na chuki.
Amesema kufikia mwaka 2022 serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo,na jamii wanahakikisha tatizo la ukatili dhidi ya wanawake na watoto linapungua kwa asilimia 50 lengo likiwa kujenga jamii yenye amani na upendo na kuleta ustawi katika maisha.
Maeneo ya utekelezaji wa mpango waTaifa katika kupinga vitendo hivyo ni kuimarisha uchumi wa kaya,mila na destuli,malezi,mazingira salama mashuleni na stadi za kazi na maeneo mengine ni usalama maeneo ya umma kwa wanawake na watoto na utoaji huduma kwa wahanga wa ukatili.
Wanawake na watoto wameipongeza serikali kwa kuanzisha kamati hiyo kwani kamati hiyo itasaidia kutatua changamoto zinazowa kabili katika jamii na wao kubaki katika hali ya usalama.
Imeandaliwa na afisa habari,mawasiliano na mahusiano serikalini
SONGEA DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa