Serikali kupitia Halmashuri ya Wilaya ya Songea inatarajia kuanza ujenzi wa stendi ya Magari (Mabasi) katika Kijiji cha Lundusi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea. Stendi hiyo itakayogharimu kiasi cha Shiling Milioni 434,657,802.68, inategemea kuanza utekelezwaji baada ya uzinduzi utakaofanyika tarehe 15/09/2023.
Akizungumzia mradi huo Mhandisi wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Flora Tairo amesema wamepokea kiasi hicho cha fedha kupitia TASAF kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao lengo kubwa ni kusaidia wananchi wa kijiji cha Lundusi na vijiji jirani katika kuondoa changamoto za usafiri.
"Stendi hii imegawanyika katika maeneo matano ya utekelezaji ambayo ni -; sehemu ya kupaki magari, Ujenzi wa Pelving blocks, Ujenzi ufungaji wa taa pamoja na ujenzi wa maduka, ambapo maduka yatakuwa katika sehemu mbili (side A na side B)".
"Hatua za utekelezaji wa mradi, tulianza na uibuaji wa mradi, tukaja uhakiki wa mizani, pia tukafanya uhakiki wa eneo la mradi, tukafanya uhidhinishaji wa maombi ya fedha za mradi na utafuata uzinduzi wa mradi na utekelezaji wa mradi kwa sasa tupo hatua hii ya utekelezaji wa mradi ambapo mradi wetu upo katika hatua za awali za ujenzi huo ambapo sasa ni usafishaji wa eneo (site clearance) baada ya hapo kutakuwa na utekelezaji wa miundombinu katika stendi yetu baada ya utekelezaji wa mradi tutakuwa na kukamilika kwa mradi baada ya kumaliza mradi wa miundombinu kutakuwa na cheti cha umalizaji wa mradi na ufunguzi wa mradi huo". Flora Tairo Mhandisi wa Halmashuri
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndg. Neema M Maghembe ameeleza namna mradi huu utaweza kuwanufaisha wananchi wa kijiji cha Lundusi na vijiji jirani ambao watatumia stendi hiyo pindi itakapo kamilika vilevile ameishukuru Serikali kwa kuweza kuwapatia fedha za mradi, amapo amesema.
" Katika mapokezi ya fedha hizi, kwanza kabisa tunampongeza Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazozifanya pia tunamshukuru kwa kutuletea fedha hizi kwaajili ya utekelezaji wa mradi huu wa stendi na miundombinu mingine katika Halmashauri yetu, Tunamshukuru pia Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mh Jenista Joakim Mhagama kwa ufuatiliaji mzuri na kazi nyingi anazozifanya katika Jimbo lake, Mkurugenzi wa TASAF Makao Makuu, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa ushari na ufuatiliaji wake, Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mwenywekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Mhe. Menans Komba na baraza lote la Madiwani na timu ya wataalamu katika usimamizi wa utekelezaji wa miundombinu hii bila kusahau Chama Cha Mapinduzi kwa mchango wake mkubwa katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Songea"
“Nasi tunawaahidi kushirikiana vyema na kamati zote zilizopo hapa katika utekelezaji wa mradi huu ambao utaenda kunufaisha watu wengi sana ili kuhakikisha kwamba fedha hizi zilizoletwa na Mheshimiwa Raisi kupitia TASAF zinaenda kufanya kazi iliyokusudiwa”
Aidha uzinduzi wa mradi huu unatakiwa kufanyika Tarehe 15 September 2023 kwani utekelezaji wa miradi ya miundombinu kupitia TASAF huanza kwa zoezi la uzinduzi kabla ya utekelezaji wa mradi kwa Lengo la kuwapa wananchi taarifa ya mradi na hamasa juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya stendi katika Kijiji cha Lundusi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa